March 10, 2018




Baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amewatuliza mashabiki kwa kusema bado wanayo nafasi ya kusonga mbele.

Jumanne wiki hii Yanga ilishindwa kutamba kwenye Uwanja wa Taifa na kufungwa Township Rollers na timu hizo zitarudiana Machi 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Gaborone, Botswana.

Ajibu  amesema bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano hivyo mashabiki wao wasikate tamaa na wawasamehe kwa matokeo mabovu ya awali.

 “Bado tunayo nafasi na tunaweza pia nina imani tutawafunga wapinzani wetu nyumbani kwao kikubwa ni kuendelea kutusapoti na sisi tutapambana ili kuweza kupata matokeo.

“Najua mashabiki wetu wameumia kwa matokeo yale, ila hatuna budi kuwaomba msamaha, watusaheme na nafasi ya kufanya vizuri bado tunayo wasikate tamaa,” alisema Ajibu.


Hata hivyo, Yanga ili ifuzu inahitaji ushindi wa uwiano wa mabao 2-0 ili iweze kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kama ikitolewa itaangukia katika kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. 

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Ajibu kwani mmekosa nini ndio uombe msamaha? Huo ni mchezo wa mpira, hamjafanya makusudi. Mmejitolea uwezo wenu wote pale ndipo mlipofikia mwisho wa jitihada zenu. Mnapaswa kupongezwa kwa kilichopatikana. Muhimu gangeni mechi ijayo ili mshinde.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Exactly....ila kama mchezaji anayo haki ya kutuomba radhi mmashabiki kwa sababi ni kweli tulikatishwa tamaa na matokro yale hasa ukizingatia tulikuwa home. Big up ajibu kwa kujitambua tupo pamoja nanyi yanga mbele daima nyuma mwiko....

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic