LIVERPOOL HOI MBELE YA UNITED, YALAZWA MABAO 2-1 OLD TRAFFORD
Manchester United imezidi kuonesha ubabe wake kwa Liverpool, baada ya kuitandika mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford leo, mechi ya Ligi Kuu England.
United imepata mabao yake kupitia Marcus Rashford, aliyefunga katika dakika za 14 na 24 kipindi cha kwanza.
Hadi dakika 45 za awali zinamalizika, United ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Licha ya kutawala kwa asilimia kubwa katika dakika zote 90, Liverpool ilifanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Eric Bailly kujifunga ikiwa ni dakika ya 66, baada ya kushindwa kuokoa mpira a krosi uliopigwa na Sadio Mane.
United sasa imeendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na alama 65 dhidi ya Liverpool yenye 60.
0 COMMENTS:
Post a Comment