Straika wa zamani wa Yanga, Aaron Nyanda, ametoa maoni yake kuhusu kupungua kwa ushawishi wa mashabiki wa kitanzania kwenda viwanjani tofauti na zamani.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na hamasa ndogo ya mashabiki kwenda viwanjani kutazama mechi zinachochezwa, ilihali enzi za nyuma haikuwa hivyo.
Nyanda amesema moja ya sababu ni huu mfumo wa kielektroniki kuanzishwakua na baadhi ya mapungufu.
Akizungumza na kipindi cha Sports Extra kupitia Clouds FM, Nyanda ameeleza utaratibu wa tiketi za kielektroniki umekuwa si mzuri na unaleta usumbufu kwa watu kuingia Uwanjani.
"Tiketi za kielektroniki zimekuwa sababishi kutokana na utaratibu wake kutokuwa mzuri, hii inasababisha watu wapatwe na uvivu wa kwenda Uwanjani" amesema Nyanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment