March 2, 2018



Na George Mganga

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, ana hatuhati ya kucheza mchezo wa leo kutokana na hali yake kiafya kutokuwa sawa.

Okwi aliumia katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Mbao FC uliochezwa Jumatatu ya Februari 26 2018 katika Uwanja wa Taifa, dar es Salaam.

Licha ya taarifa ya Simba iliyoarifu kuendelea vizuri kwa mchezaji huyo, mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu kurejea sawa kwa mchezaji huyo, na haijajulikana kama atacheza dhidi ya Stand United leo au la.

Ripota wa Saleh Jembe alipojaribu kumtafuta Haji Manara, alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwani lipo juu ya Mwalimu na Daktari wa timu kama ataweza kucheza leo ama, japo akasema atalitolea ufafanuzi kesho atakapoitisha kikao na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic