March 9, 2018


Na George Mganga

Kiungo Mkenya anayekipiga Tottenham Hotspurs, Victor Wanyama, leo ametangazwa kuwa mchezaji aliyefunga bao bora kwa mwezi Februari 2018, Ligi Kuu Uingereza.

Wanyama alifunga bao hilo walipokutana na Liverpool katika Uwanja wa Anfield Februari 4 2018 ikiwa ni dakika moja tu akitokea benchi.

Bao hilo alilomfunga kipa Loris Karius lilikuwa la kwanza kwake katika msimu huu na likiwa la kwanza kwenye mchezo huo ambao matokeo ya mechi hiyo yalienda sare ya 2-2.

Na baada ya kutwaa tuzo hiyo, Wanyama amesema hilo limekuwa moja ya mabao yake aliyowahi kufunga kwenye maisha yake ya soka.

"Hilo lilikuwa moja ya magoli yangu bora kuwahi kufunga" amesema Wanyama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic