March 1, 2018






Nyota wa zamani wa Simba na Tanzania, Abdallah Kibadeni ameendelea kusisitiza kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa kama wenyewe hawatavurugana.

Kibadeni ambaye anashikiria rekodi ya mchezaji pekee kufunga mabao matatu au hat trick katika mechi ya watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba, amesema Simba ndiyo wenye uwamuzi wa kuchukua au kutochukua.

“Nafasi waliyonayo ni kubwa snaa, timu yao iko vizuri na ni suala la wao tu kuendelea kupambana. Nafikiri hakuna wa kuwazuia Simba kuchukua ubingwa hasa kama wasipogombana wenyewe,” alisema.






Pamoja na kuichezea, Kibadeni amewahi kuinoa Simba kwa nyakati tofautitofauti.

Baada ya mechi 19, Simba wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 45 na wanafuatiwa na watani wao wa jadi Yanga wenye pointi 40.

1 COMMENTS:

  1. Simba watu wengi wadau wa soka wanawatabiria kuwa mabingwa msimu huu. Hebu fanyeni kweli acheni masihara. Chezeni mpira wa mashindano msicheze kama mpo mazoezini. Kuna wakati wachezaji wanajisahau. Mechi zenu zote zilizobakia hakikisheni mnashinda kwa mabao 2 kuendelea. Hapo mtakuwa mmejihakikishia ubingwa pasipo shaka.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic