March 1, 2018




Bao alilofunga beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy limekuwa gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka hasa wale wa mitandaoni katika magrupu mbalimbali.

Kessy alifunga bao hilo ambalo lilikuwa na ushindi wakati Yanga ikiifunga Ndanda FC kwa mabao 2-1 kwneye Uwanja wa Nangwana Sijaona mjini Mtwara na kuvunja mwiko.

Beki huyo alifunga bao hilo ‘akiwatikisa’ mabeki wa Ndanda FC kabla ya kuachia mkwaju ulikwenda kwenye ‘engo’ ya goli na kutinga wavuni.

Tokea jana usiku hadi leo asubuhi, wadau mbalimbali wamekuwa wakijadili na kusema bao hilo linapaswa kuingia kwenye moja ya mabao bora ya Ligi Kuu Bara.

Kama hiyo haitoshi, wengine wamekuwa wakisema bao hilo limefungwa na beki huku mafowadi wengi wakiwa hawafungi mabao ya namna hiyo.


Gumzo kubwa wako wamekuwa wakiamini kuna haja ya kusubiri kwa kuwa mabao mengine yatafungwa lakini wapo wanaoona hata yakifungwa kutakuwa na ugumu ya kuliondoa ndani ya tatu au tano bora ya mabao bora ya Ligi Kuu Bara.

4 COMMENTS:

  1. It was a wonderful goal

    ReplyDelete
  2. Nyie wafungaji plz plz utatengua nyonga magolikipa wetu, Jeremiah kisubi nusu ateguke kiuno

    ReplyDelete
  3. Hivi KISUBI J, hakulazwa hospitality kweli? Ile kitu ya Kessy haiwezi kumwacha golikipa salama.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic