KIKOSI CHA YANGA CHAPEWA MAPUMZIKO KABLA YA KUANZA KUJIFUA KUIKABILI SINGIDA UNITED
Kikosi cha Yanga kimepewa mapumziko ya siku mbili kuelekea maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.
Mapumziko hayo yameanza leo Jumanne mpaka kesho Jumatano ambapo siku ya Alhamis wachezaji wote watarejea kambini kuanza mazoezi.
Yanga itakuwa na mechi dhidi ya Singida United katika mashindano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika April 1 2018 kwenye Uwanja wa Namfua.
Kikosi hicho kinaenda mapumziko ya siku mbili baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Bostwana kwa jumla ya mabao 2-1.
Vilevile Yanga inaweza kuwa na mshambuliaji wake, Donald Ngoma, ambaye imearifiwa ataanza mazoezi na kikosi hicho Alhamis ya wiki hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment