YANGA YATUMA SALAAM SINGIDA UNITED, NGOMA FITI KUANZA MAZOEZI ALHAMIS HII
Na George Mganga
Baada ya kukosekana Uwanjani kwa muda mrefu, Uongozi wa klabu ya Yanga umesema Mshambuliaji, Donald Ngoma, ameshapona majeraha yaliyokuwa yakimkabili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika, amesema mchezaji huyo yupo fiti hivi sasa, na ataanza kufanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.
Nyika amesema, kwa mujibu wa daktari, Ngoma tayari ameshapona na ataanza mazoezi Alhamis ya wiki hii.
Yanga itakuwa ina kibarua April Mosi 2018 cha mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United, mechi itakauopigwa Uwanja wa Namfua, mjini Singida.
0 COMMENTS:
Post a Comment