KUJUA KAMA YANGA ITAPANGWA NA ENYIMBA, AL MASRY AU RAJA CASSABLANCA, KESHO NDIYO SIKU YA DROO
Na George Mganga
Kuelekea hatua ya makundi, droo ya upangaji wa timu zitakazokutana kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, inataraji kufanyika kesho mjini Cairo, Misri.
Droo hiyo itahusisha timu zilizoanguka kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na timu ambazo bado zipo Kombe la Shirikisho.
Tanzania ina mwakilishi mmoja pekee ambaye ni Yanga, Yanga wanasubiri kujua watapangiwa na timu ipi ambapo kuna baadhi ya vigogo mbalimbali kama Al Masry walioitoa Simba, Raja Cassablanca, Enyimba, SuperSpot United ya Afrika Kusini.
Baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga sasa itapeperusha bendera ya Tanzania kwa kuwekeza nguvu zake kwenye mashindano haya.
Kesho Machi 21 2018 ndiyo droo rasmi itafanyika ili kujua itapangwa kucheza na klabu gani.
0 COMMENTS:
Post a Comment