MPIRA UMEKWISHAAAAAA
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 90 Simba wanashambulia mfulilizo, Masry wanaokoa
Dk 90 OKwi anajaribu kuingia anazuiwDk 89 kipa kajilaza pale kupoteza muda
Dk 88 Okwi anaaachia mkwaju unawababatiza mabeki na kuokolewa
KADI dk 87 Bocco anapewa kadi ya njano
SUB Dk 85 Yusuf Otara anaingia kuchukua nafasi ya Islam Issa
Dk 83 Glindo anawachambua mabeki wawili wa Simba na kuachia krosi lakini wanapoteza nafasi
Dk 81 Bance anapiga kichwa hapa na Manula anadaka vizuri
KADI Dk 80 Juuko analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Gomaa ambaye bado yuko cchini pale
Dk 80 Bocco anaruka vizuri hapa lakini kipa anaokoa hapa
Dk 79 Mavugo ndani ya 18, anaachia mkwaju mkali lakini kipa anaonyesha ujuzi mkubwa anadaka ilikuwa nafasi nzuri zaidi kwa Simba katika mchezo huu
Dk 78. Mkude anaachia mkwaju mkali hapa lakini hakulenga
Dk 75, Simba wanaonekana kuanza kufunguka, wanashambulia na Gyan anaachia mkwaju mkali hapa lakini goal kick
SUB Dk 73 Simba wanamtoa Kotei na nafasi yake inachukuliwa na Shiza Kichuya
Dk 72 Kotei anafanya kazi ya ziada kumzia bance na mpira unakuwa wa kurushwa
Dk 71, Simba wanaonekana kuanza kufunguka na kushambulia
Dk 69 Okwi anaingia vizuri na kuachia mkwaju mzuri hapa, mabeki wa masry wanaondosha hatari
Dk 68 sasa, Gyan naye yuko chini pale akitibiwa huku mashabiki wa Masri wakiendelea kuzomea
Dk 67 Kotei naye anafanyiwa madhambi, mwamuzi anasema sijaona twende. Wachezaji wa Simba wanaonekana kukasirishwa wanamfuata mwamuzi na yeye anamuita Okwi na kumuonya asiendele kumlaumu. Kotei bado anatibiwa
Dk 67, Okwi anawekwa chini, mwamuzi anasema twende, sijaona
SUB Dk 66, Simba wanafanya mabadiliko, anaingia Mavugo kuchukua nafasi ya Mlipili
Dk 63, Manula anagonjwa wakati akijaribu kuokoa na sasa yuko chini na mchezaji mmoja wa Masry yuko chini pia
Dk 61 Kwasi anajaribu mkwaju, goal kick
Dk 59 hatari kwenye lango la Simba, mpira unatoka pembeni kidogo
Dk 59 Mohammed wa Masry anajiangusha na mwamuzi anasema faulo
Dk 56, Gyan anaachia mkwaju mkali kabisa, unatoka pembeni kidogo ya lango la Masry, ilikuwa hatari
Dk 55 hatari kwenye lango la Simba, Manula anagongwa lakini mwamuzi hakuona huenda, mpira unapigwa lango la Simba likiwa tupu, goal kick
Dk 54 inachongwa faulo, Gyan anaokoa na kuwa kona ya kwanza kipindi cha pili
KADI DK 53 Mkude anaonyeshw akadi ya njano kwa kumuangusha Mohammed
Dk 51, Manula anafanya kazi ya ziada kuruka na kuokoa mpira juu ya kichwa cha Mustapha
Dk 51 sasa, Masry wanaonekana kuwa na kasi lakini bado Simba wanalinda zaidi
Dk 49, Manula anaruka na kuokoa, ilikuwa hatari kabisa
Dk 48 Masry wanapata faulo karibu kabisa na lango la Simba, si eneo salama
Dk 47 Nyoni anaruka vizuri na kuokoa
Dk 45, kipindi cha pili kimeanza na Masry wanaonekana kushambulia kwa kasi. Lengo ni kupata bao la mapema
MAPUMZIKO
KADI Dk 44 Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Glindo
Dk 43 kuna faulo karibu kabisa na Simba baada Kotei kugongana na Gomaa wakati wakiwania mpira
Dk 41 kuna vurugu zinaendelea na wachezaji wanafukuzana na kurushiana mikono mpira umezimama
Dk 39, Mlipili analazimika kumlza chini Salam katika eneo hatari baada ya Gyan kupoteza mpira
Dk 36 Bance anawachomoka Simba, anaachia mkwaju mkali hapa, Manula anadaka kwa ustadi
Dk 36 Gomaa anaingia vizuri lakini Juuko anaokoa na kuwa kona, inachongwa Kotei anapiga kichwa manula anauwahi
Dk 35 kona inachongwa Kwasi anaruka na kuokoa, kona tena inachongwa Simba wanaokoa
Dk 34, bado Masry wanapata kona baada ya krosi hatari kabisa
Dk 30 Masry wanapata kona ya kwanza, inachongwa hatariiii, goal kick
Dk 29 Bance anakwenda vizuri lakini Mkude anamuwahi na kuchukua mpira
Dk 28, kipa Masry anaruka juu na kuudaka mpira kama nyani baada ya krosi ya Gyan
Dk 27, Okwi anawekwa chini hapa na mpira unapigwa kwenda Masry
Dk 26 Manula anafanya kazi ya ziada kudaka mpira mbele ya Mustapha, ilikuwa krosi hatari ndani ya lango la Simba
Dk 25, hatari kwenye lango la Simba lakini Manula anaruka na kudaka mbele ya Bance
Dk 23 mpira umesimama, Gyan amegongana na Hamty wa Al Masry na wote wanatibiwa
Dk 21, Bocco anaingiza krosi safi kabisa lakini Okwi anachelewa na mpira unakuwa goal kick
Dk 20 Manula analala chini pale inaonekana aliumia wakati aliporuka kuokoa
Dk 19 krosi hatari ndnai ya lango la Simba lakini Mkude anaruka vizuri na kuokoa
Dk 17, krosi safi ndani ya lango la Simba lakini Simba wako makini, mpira ni goal kick
Dk 15, Okwi alimchambua beki na kutoa pasi kwa Kapombe lakini alikuwa amevutwa na kuangushwa
SUB Dk 12 anaingia Bance kuchukua nafasi ya Ahmed Gomaa aliyeumia
Dk 12, mpira umeanza na yule mchezaji ametolewa
DK 11 bado mchezaji yule hajatolewa na Manula amekuwa akimulikwa na mwanga wa kijani ili kumchanganya, hawa ni mashabiki
Dk 9, kuna mchezaji wa Al Masry yuko chini, tatizo la nyama, MPIRA UMESIMAMA
Dk 8 Kapombe anatolewa nje kwa ajili ya kutibiwa zaidi
Dk 7, mpira mkali wa faulo, Kapombe anaokoa kwa kichwa na sasa yuko chini pale, anaanza kutibiwa
Dk 6, kuna faulo karibu kabisa na lango la Simba, ni hatariDk 6 sasa, Simba wamerudi nyuma na wanalinda zaidi ya kushambulia
Dk 3, Simba wanamuachia Mohammed kupiga kichwa akiwa peke yake, hakulenga
Dk 1 Mechi imeanza na Masry wamekuwa wa kwanza kufika katika lango la Simba. Manula yuko makini
Ahsante Sana Simba mmepambana, kazi tumeiona goli la ugenini limewatoa siyo mbaya
ReplyDeleteAhsante Sana Simba mmepambana, kazi tumeiona goli la ugenini limewatoa siyo mbaya
ReplyDelete