LIVE UPDATES: FLL TIME: ALGERIA 4-1 TAIFA STARS, MCHEZO WA KIRAFIKI KIMATAIFA
MPIRA UMEKWISHA, ALGERIA 4-1 TAIFA STARS
Dak ya 90+1, Mpira unarushwa kueleka Algeria
DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, TATU ZIMEONGEZWA
Dak ya 89, Bado dakika moja pekee, kadi ya njano inaenda kwake Yondani baada ya kucheza madhambi
Dak ya 88, Stars namna gani leo, wanakosa kujifunga tena hapa. Wanaokoa, mpira unasonga mbele
Dak ya 87, Stars wanao hivi sasa, Algeria wanapokonya na kuutoa nje, unarushwa na Stars
Dak ya 86, Msuva anapigaa, mpira unakwenda nje
Dak ya 85 Samatta anapiga kona fupi kwa kumpasia Msuva, anafanyiwa madhambi, faulo,
Dak ya 85, Bado mpira umesimama
Dak ya 84, Mpira umesimama tena. Mchezaji wa Algeria ameumia, dakika zinazidi kuyoyoma
Dak ya 83, Mpira umesimama kidogo, Algeria wanafanya mabadiliko, Samatta anapiga lakini kipa anapangua na mpira unakwenda nje, kona
Dak ya 82, Kipa Mohammed anapiga mbele huku unamkuta Samatta, faulo, anapiga Samatta
Dak ya 82, Ni goli kiki, Stars wanaanza upya
Dak ya 81, Samatta anatoa mpira nje, unarushwa kuelekea Stars
Dak ya 79, Goooli, Bao la 4 wanapata Algeria
Dak ya 79, Zimesalia dakika 11 mpira umalizike
Dak ya 76, Mbwana Samatta anapewa kadi ya njano
Dak ya 75, Nafasi wanaipata Stars, lakini mabeki wa Algeria wanakuwa wengi na kuukoa mpira
Dak ya 73, Offside, Stars wanaotoea
Dak ya 72, Kazi nzuri ya Mohammed inasaidia kuokoa bao la nne baada ya kudaka shuti kali la mshambuliaji wa Algeria
Dak ya 71, Stars wanatoa mpira mpira, unarushwa kuelekea kwao
Dak ya 67, Algeria wanafanya mabadiliko, anaingia Ghafai na Rami anatoka
Dak ya 66, Hatarii, Gadiel Michael anapiga mashuti mawili makali kushoto wa Uwanja lakini kipa wa Algeria anakuwa mahili anapangua yote
Dak ya 65, Matokeo ni 3-1 mpaka sasa
Dak ya 63, Algeria wanamiliki mpira kwa asilimia kubwa, Stars wanapambana kutafuta bao la pili
Dak ya 62, Stars wanafanya mabadiliko, anaingia Nyoni kuchukua nafasi ya Mudathir Yahaya
Dak ya 60, Wnakwenda sasa Stars, Gadiel na mpira kushoto mwa Uwanja, anajaribu kupiga krosi, anapiga lakini inatolewa nje, kona. Kona inapigwa na mpira unaokolewa
Dak ya 59, Hataari, ngonga gonga nyingi za waarabu zimesababisha kukosa bao la 4 kwa Algeria
Dak ya 58, Hali imekuwa ngumu kwa Stars, waarabu wanatawala na mpira muda wote. Wanatafuta mabao zaidi
Dak ya 54, Stars wanaanza upya tena kati, yaonekana hakuna mipango mbadala kwa Mwalimu Mayanga kupindua matokeo, Algeria wametawala zaidi
Dak ya 53, Goooli, Stars wanafungwa bao la 3
Dak ya 52, Almanusra Stars wajifunge tena, Mohammed anadaka mpira
Dak ya 50, Algeria wanakwenda kushoto mwa uwanja, wanashumbulia, hatarii, pigwa krosi moja Banda anaokoa, inapigwa tena nyingine, mpira unakwenda nje
Dak ya 49, Mpira upo langoni mwa Stars, wameanza upya
Dak ya 48, Mabao ni 2-1
KIPINDI CHA PILI KIMEANZA
MAPUMZIKO: DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA
Dak ya 45, Faulo inapigwa kuelekea Algeria, Kichuya anapiga, piga pale, mpira unapaa juu ya lango
DAKIKA MOJA IMEONGEZWA KUELEKEA MAPUMZIKO
Dak ya 43, Goooli, Kapombe anaizawadia Algeria bao la pili baada ya kujifungwa kwa njia ya kichwa
Dak ya 43, zimesalia dakika 2 kwenda mapumziko
Dak ya 40, Hatari kwenye lango la Stars, inapigwa krosi huku, kichwa kinapigwa lakini kinakuwa fyongo
Dak ya 38, Algeria wametoa, Gadiel anarusha, cheza kwake Kichuya lakini anachezewa madhambi, mpira unapigwa kuelekea Algeria
Dak ya 38, Mpira umekuwa mwingi kwa waarabu, wametala zaidi eneo la kati
Dak ya 37, Offside, mshambuliaji wa Algeria anaotea
Dak ya 36, Matokeo bado ni 1-1
Dak ya 35, Algeria wako eneo la kati mwa Uwanja, wanajaribu kutengeneza nafasi ya kupenya ngome ya Stars
Dak ya 33, Stars wanatengeneza nafasi nyingine nzuri na wanashindwa kuitumia
Dak ya 32, Msuva sasa anashambulia, anakwenda, piga pasi lakini mabeki wa Algeria wanauwahi
Dak ya 31, Mahrez sasa anaukokota kulia mwa Uwanja, Gadiel anamnyang'anya, pigwa mbele huku, unatoka
Dak ya 30, Algeria wanapata kona, inapigwaa, mabeki wa Stars wanaokoa
Dak ya 29, Algeria wanachukua tena mpira sasa, wanarejesha nyuma kwa kipa kuanza upya
Dak ya 28, Stars wameonekana kuamka sasa baada ya kusawazisha
Dak ya 27, Gadiel anarusha mpira baada ya kutolewa na wapinzni, wanatoa na anarusha tena
Dak ya 25, Kocha wa Algeria kama haamini hivi, muda wote amesimama
Dak ya 24, Banda anarusha, unatolewa tena. Anarusha tena kwake Samatta lakini anakwenda chini
Dak ya 23, Algeria wanaanza tena upya golini mwao, Kichuya anamgongeshea mshambuliaji wa Algeria na anautoa nje mpira, unarushwa kuelekea kwao
Dak ya 22, Inapigwa pale, kichwa kinagongwa na kipa anadaka
Dak ya 21, Hatari nyingine langoni mwa Stars, mabeki wanaokoa na mpira unakwenda nje, kona
Dak ya 21, Faulo inapigwa kuelekea Stars
Dak ya 20, Goooooli, Msuva anaisawazishia Stars kwa njia ya kichwa baada ya kona nzuri kutoka kwa Kichuya kumfikia
Dak ya 19, Hatari katika lango la Algeria, Stars wanafanya shambulizi lakini mpira unakwenda nje
Dak ya 18, Algeria wanakosa bao la pili, mpira wa wazi unakwenda nje kufuatia shambulizi zuri
Dak ya 17, Kocha Mayanga amesimama kutoka kwenye benchi
Dak ya 17, Free Kiki, inapigwa kuelekea Stars
Dak ya 15, Faulo inapigwa kuelekea Algeria, mpigaji Samatta, anapigaaa, mabeki wanaokoa
Dak ya 14, Algeria wameutawala Uwanja, Samatta sasa anauchukua mpira kushoto mwa Uwanja, kwenda na mpiraaa huku, anapiga lakini kipa anaokoa na mguu
Dak ya 12, Stars wameweka mpira kati kuanza
Dak ya 12, Algeria wanapata bao la kwanza, ngome ya Stars imeonesha udhaifu
Dak ya 10, Kipa Abdulrahman Mohammed leo ana kazi ya ziada kufanya
Dak ya 9, Stars wanapambana kuusaka mpira, bado milango ni migumu
Dak ya 7, Bado Algeria wanaumiliki kwa wingi, wametawala eneo la kiungo
Dak ya 56, Algeria wanaumiliki zaidi mpira kwa takribani dakika 6 za mwanzo, Samatta anapata nafasi, anadondoka, Algeria wanauchukua mpira
Dak ya 4, Pigwa krosi nyingine tena, kipa Mohammed anaokoa kwa kudaka mpira
Dak ya 3, Hatari langoni mwa Stars, inakuwa ni kosakosa ya pili kwa waarabu, wanajaribu kutafuta bao la mapema
Dak ya 2, Algeria wanaanza eneo la nyuma, wanapasiana
Dak ya 1, Mpira umeanza. Algeria wanapata shambulizi la kwanza, wanakosa
Tanzania na gambling ya makocha sijui tutaacha lini?...Hawo Mayanga na Hemedi Morocco hawana level ya kufundisha timu ya Taifa.Waishie kufundisha timu za ligi zetu. TFF tuleteeni makocha wa viwango.....
ReplyDelete