March 24, 2018


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, ameeleza kutofurahishwa na matokeo waliyoyapata dhidi ya Algeria katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Alhamis ya wiki hii.

Katika mchezo huo ambao Stars ilikubali kipigo cha mabao 4-1, kimemfanya Kocha Mayanga aanze mapambano ya kutuliza presha ya Watanzania dhidi ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo watakapocheza nayo Machi 27 2018 jijini Dar es Salaam.

Mayanga amesema watatumia makosa ambayo yalionekana katika mchezo huo ili kufanya marekebisho kabla ya kukabiliana na Congo.

"Ni kweli mchezo ulikuwa mgumu kwetu kutokana na ubora wa timu zote mbili, tutatumia makosa ambayo yalionekana kwenye mechi yetu na Algeria kabla hatujakutana na Congo ili tusipoteze tena" alisema.

Hata hivyo Mayanga ameshukuru kupata mchezo mkubwa kama ule wa dhidi ya Algeria akieleza kuwa ni kipimo kizuri ukilinganisha ubora wa timu zote mbili zilivyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic