March 4, 2018


Lionel Messi ameendeleza ubabe wa kufunga mabao ya free kiki baada ya kuisaidia FC Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid.

Messi amefunga bao hilo katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo uendeke dakika 45 za mwanzo matokeo yakiwa ni 1-0.

Kipindi cha pili kimeshuhudiwa bila kuona nyavu zikichezwa huku bao la Messi likidumu kwa dakika zote 90.

Kwa matokeo hayo Barcelona imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 69 dhidi ya 61 za Atletico Madrid.

Messi pia ameweka rekodi ya kufunga bao la 600 akiwa na FC Barcelona baada ya kufunga leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic