MZEE AKILIMALI AITAKA YANGA IITISHE UCHAGUZI ILI KASI YA MABADILIKO IWEPO
Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameuomba uongozi wa timu hiyo kuitisha uchaguzi huku akisema hapingi mabadiliko.
Akizungumza na ripota wa Saleh Jembe, Mzee Akilimali amesema Yanga haina Mwenyekiti mpaka sasa, na badala yake ni vema ikaitisha uchaguzi ili mabadiliko yaende kasi.
Akilimali ambaye amekuwa akilipigia kelele suala kwa muda mrefu, anaamini pale Mwenyekiti atakapopatikana, mchakato wa mabadiliko utaenda vizuri.
Aidha, Akilimali ameeleza kuwa, Mwenyekiti wao wa zamani Yusuph Manji, tayari alishajiondoa hivyo ni vema akapewa muda apumzike na endapo akitaka arudi anakaribishwa.
Manji alijiudhulu nafasi ya Uenyekiti ndani ya Yanga baada ya kukumbukwa na mashtaka ya kesi ikiwemo la Uhujumi Uchumi mwaka 2017.
0 COMMENTS:
Post a Comment