KOCHA STAND: HATA KAMA ANGEKUWEPO OKWI, SIMBA WAKIKAZA SANA WANAONDOKA NA ALAMA MOJA
Na George Mganga
Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal Bilo, ametamba kuipiga STOP Simba kuzidi kujipatia alama ambazo zitaifanya iendelee kuwa juu ya kilele cha msimamo wa ligi.
Bilo ambaye timu yake inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuikabili Simba leo, amesema maandalizi yao vako vizuri pamoja na molari ya wachezaji, hivyo anaamini watashinda.
Aidha Bilo amesema kukosekana kwa mshambuliaji wao Emmanuel Okwi hakutawanyima chochote huku akieleza haoni jipya kwani walishawahi kucheza na Simba iliyokuwa na Marehemu Mafisango.
Bilo ametamba kuwa Simba ya sasa haina kipya, huku akijidai kwa kueleleza kuwa kama wakijitahidi sana, basi wataambulia alama moja na si 3.
Ametabiri sawa lakini si kwamba timu yake imecheza kuliko Simba hapana. uwezo wa umiliki mpira umeonyesha Simba walimiliki kwa asilimia nyingi zaidi ila matokeo ni hayo aliyoyatabiri kocha wa Stand united, kugawana pointi.
ReplyDeleteBaba mpira magoli
Delete(h)
ReplyDelete