March 10, 2018


Nyota Cristiano Ronaldo amezidi kuonyesha ubora wake baada ya kuifungia Real Madrid mabao 2 dhidi ya Eibar kwenye La Liga.

Mchezo huo uliopigwa Ipurua Municipal Stadium umemalizikwa kwa jumla ya mabao 2-1.

Ronaldo alianza kuifungia Madrid dakika ya 34 kabla ya Eibar kusawazisha kupitia Ivan Ramis katika dakika ya 50.

Mnamo dakika ya 84 tena Ronaldo aliingia kambani kwa mara ya pili na mpaka mchezo unamalizika Madrid walikuwa mbele kwa mabao hayo.

Mabao hayo mawili aliyofunga Ronaldo, yanamfanya afikishe 18 msimu huu katika Ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic