March 30, 2018






Tayari kuna taarifa mabingwa wa soka Tanzania, Yanga, wameanzakimyakimya harakati zake za usajili kwa kumuwahi kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahaya ambaye anatajwa kwa sasa kuwa amemaliza mkataba wake na klabu hiyo.

Kiungo huyo ambaye anacheza kwa mkopo Singida United akitokea Azam FC, inaelezwa kuwa, mkataba wake na Azam ulimalizika tangu mwanzoni mwa mwezi huu huku kukiwa hakuna makubaliano ya mkataba mpya.

Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinasema, vigogo wa timu hiyo wameshazungumza na kiungo huyo, hivyo
wanasubiriwa kipindi cha usajili kifike wakamilishe mchakato huo.

Wakati mchakato huo kwa upande wa Yanga ukiendelea, Azam wameibuka na kutolea ufananuzi juu ya mchezaji huyo ambaye alianza kuitumikia klabu yao kuanzia timu yao ya vijana chini ya miaka 15.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd, alisema: “Mkataba
wa Azam na Mudathir umemalizika mwezi huu, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru ambaye anaweza kuzungumza na timu yoyote ambayo anaona ina maslahi kwake.

“Kwa upande wetu tunaweza kusema Mudathir ni kijana ambaye tulikuwa naye tangu kikosi cha vijana chini ya miaka 15, mpaka amekuja kupandishwa timu ya wakubwa ambapo kwa ubora wake akajumuishwa kwenye kikosi cha
timu ya taifa ya Tanzania. Tunamtakia kila la heri popote ambapo ataelekea.”

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika, amezungumzia usajili wa kiungo huyo kwa
kusema: “Kwa sasa tupo bize na maandalizi ya mechi yetu ijayo ya Kombe la FA, masuala ya usajili yatakuja baada ya kupokea ripoti ya mwalimu mwishoni mwa msimu.

“Hivyo, kama tukianza kuzungumzia usajili katika kipindi hichi tutakuwa tunachanganya mambo, hivyo tungojee muda wa usajili ufikie ndiyo nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia hilo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic