March 23, 2018



Ungozi wa benchi la ufundi la Simba umeweka sheria kali ambapo kila mchezaji akichelewa kwenye matukio maalum anakatwa shilingi laki moja.

Uongozi huo chini ya kocha Pierre Lechantre umeweka sheria hiyo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa timu hiyo inakuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Sheria hiyo ya Simba inasema kuwa kama mchezaji akichelewa kula, akichelewa mazoezini, akichelewa kwenye basi na sehemu nyingine muhimu anakatwa kiwango hicho cha fedha.

“Huu ni utaratibu wetu kwa muda mrefu kidogo kuanzia benchi hili la ufundi limeanza kazi.
“Wachezaji wanatakiwa kuwahi sehemu zote muhimu, kila sehemu hata Ulaya wachezaji wanatakiwa kula pamoja, wanatakiwa kuwahi kwenye basi na mazoezini.

“Utaratibu huu umeleta nidhamu ya hali ya juu klabuni, ndiyo maana umeona timu inafanikiwa kwa sasa kwa kuwa kuna nidhamu ya hali ya juu sana kwa sasa.

“Kama kwenye chakula na sehemu nyingine kocha ndiye amekuwa akimwita meneja na kumwambia mkate mchezaji fulani shilingi 100,000, hii ni faida kubwa kwetu,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo, kuanzia utaratibu huo umeanzishwa inaelezwa kuwa mchezaji anayeongooza kwa nidhamu ni Shiza Kichuya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic