March 23, 2018

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau akiwa na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Championi
alipotemebelea ofisi za Global Publishers hivi karibuni


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika wazi vigezo vipya watakavyovizingatia mara baada ya kuanza rasmi kupitia ‘CV’ mbalimbali walizopokea zitakazowafanya kumpata kocha mpya atakayechukua mikoba ya kocha wa sasa, Salum Mayanga.

TFF inaingia katika mchakato wa kutafuta kocha mpya baada ya mkataba wa kocha wao wa sasa Mayanga kumalizika tangu mwezi uliopita, huku akiendelea kukitumikia kikosi hicho kwa maombi maalumu.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, alisema pamoja na Mayanga kuendelea kuitumikia Stars kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya Fifa, mkataba wake ulishamalizika, hivyo TFF tayari ipo katika mchakato wa kuhakikisha inampata kocha mpya ambaye atakuwa na vigezo vya kuifikisha Stars katika anga za juu.

“Uongozi kwa sasa umejipanga kikamilifu kuhakikisha soka letu linafika mbali na ndiyo maana utaona karibia michuano yote ya kimataifa vikosi vyetu vya taifa vinashiriki na TFF inafanya kila liwezekanalo ili tuweze kufuzu kwa kila hatua inayoendelea mara tu baada ya kuingia katika michuano yoyote iliyo mbele yetu.

“Lakini kama hilo halitoshi, TFF tumejipanga kuhakikisha tunampata kocha mwenye CV kubwa zaidi ya aliyepo na kama atakosekana mwenye vigezo vya kumzidi Mayanga basi hatutakuwa na haja ya kutafuta kocha mpya.
“Kwa kuwa walimu wapo wengi wenye viwango, itategemea na hao wanaopitia majina maana makocha ni wengi.

“Kama unavyojua mwingine anaweza akapatikana na asiwe tayari kuja bila maelewano na timu yake hivyo zoezi la kumtangaza litategemea na muda utakaotumika kukamilisha mambo yote hayo,” alisema Kidau.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic