Na George Mganga
Wakili wa aliyekuwa Makamu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Emmanuel Muga, amesema amesikitishwa na maamuzi ya shirikisho hilo kumtangaza Athumani Nyamlani kuchukua nafasi ya Wambura hayajawa sahihi.
Muga ameeleza kitendo cha maamuzi hayo kufanyika ni uvunjifu wa katiba kwani kamati tendaji haikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.
Kutokana na uteuzi huo wa Nyamlani, Muga amesema watatumia utaratibu mwingine wa kutafuta haki yao ili isikilizwe hata kama itakuwa ni sehemu nyingine.
"Kwanza niseme nimesikitishwa na maamuzi ya TFF kumtangaza Nyamlani kukaimu nafasi hiyo, Kamati iliyohusika na maamuzi haikuwa sahihi kwani imevunja katiba. Sisi tutatafuta haki yetu mahala pengine hata kama itakuwa nje ya TFF' amesema Muga.
Ikumbukwe Wambura tayari alishakata rufaa rufaa ambayo mpaka sasa haijasikilizwa, hivyo Muga ameeleza kuwa wanaweza kwenda sehemu nyingine kupata haki yao.
SOURCE: SPORTS HQ, EFM
0 COMMENTS:
Post a Comment