March 26, 2018


Mhariri Mkuu Mtendaji wa Gazeti la Championi, Saleh Ally, ametoa mtazamo wake kuhusiana na Athumani Nyamlani aliyeteuliwa na TFF kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo.

Nyamlani ametangazwa kukaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa akishika wadhifa huo, Richard Wambura, kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kutumia cheo chake vibaya kwa kujipatia fedha haramu.

Kutokana na uteuzi huo, Ally amesema kuwa hana hofu kama atashindwa kuutumia wadhifa wake vizuri kwenye nafasi aliyochaguliwa kukaimu,  lakini kama amechaguliwa kwa njia na taratibu sahihi, basi aitumie nafasi hiyo hiyo kiufasaha.

"Mimi sina hofu na kuchaguliwa kwake, kama amewekwa pale kwa njia sahihi, basi afanye kazi kiufasaha'' amesema Ally wakati akizungumza na Sports HQ ya Radio EFM.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ilitangaza kumfungia maisha kutojihusisha na mchezo wa mpira wa miguu Richard Wambura, Machi 15 2018.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic