March 26, 2018


Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ameshindwa kuvumulia kelele zinazoendelea mitandaoni baada ya kusema rasmi hamuhitaji mchezaji Paul Pogba kwenye kikosi chake.

Kauli hiyo imekuja kutokana na wawili hao kuteka vichwa vya habari kwa muda mrefu kuwa hawana mahusiano mazuri.

Taarifa zinaeleza kuwa Mourinho ameitaka klabu yoyote inayomuhitaji mchezaji huyo iweke ofa mezani ili wakubaliane maana hana mpango naye.

Toni Kroos ametajwa kama mbadala anaywezeka kurithi nafasi ya Pogba kwenye kikosi cha United endapo ataondoka klabuni hapo.

Pogba alijiunga na mashetani hao wekundu mwaka 2016 kwa dau la uhamisho wa dunia wa £89m.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic