March 23, 2018



Na George Mganga

Kufuatia kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Township Rollers ya Bostwana, Yanga sasa inaweza kutwaa mpunga mwingine nje ya bilioni 1.3.

Yanga ilikuwa kidogo ibebe kitita hicho cha bilioni 1.3 baada ya kushindwa kuwang'oa Township Rollers na badala yake ikakubali kichapo cha mabao 2-1 na kuondoshwa kwenye mashindano.

Klabu hiyo ambayo imepangwa kucheza na Welayta Dicha ya Ethiopia iliyowaondoa Zamalek ya Misri kwa njia ya mikwaju ya penati, itachukua kiasi cha milioni 600 endapo itaingia hatua ya makundi kwa kuwafunga Waethiopia hao.

Yanga ilipangwa kucheza na Welayta Dicha baada ya Droo ya Upangaji wa timu zitakazokutana kwenye michuano hiyo kufanyika Machi 21 2018.

Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Aprili 6, 7 au 8, na ile ya marudiano itachezwa Aprili 17 mpaka 18 mwaka huu 2018.

Kama Yanga wakionesha ukomavu dhidi ya Welayta Dicha, basi watabeba kitita hichi cha pesa na kutumika kwa ajili ya maendeleo ya timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic