YANGA KUREJEA MAZOEZINI IKIJIANDAA KUKIPIGA NA SINGIDA UNITED, NGOMA NDANI
Kikosi cha Yanga kinatarajia kurejea mazoezini Jumatatu ya wiki ijayo, kufuatia mapumziko mafupi waliyopewa wachezaji.
Uongozi wa Yanga ulitangaza kutoa mapumziko kwa wachezaji wake, Jumatano ya wiki hii, ambapo Jumatatu wataanza rasmi maandalizi kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Yanga itakuwa ina kibarua kigumu dhidi ya Singida United katika Kombe la FA utakaopigwa mjini Singida kwenye Dimba la Namfua Aprili Mosi 2018.
Kuelekea mchezo huo, Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma, naye ataungana na wachezaji wenzake Jumatatu kama ilivyoarifiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika.
0 COMMENTS:
Post a Comment