April 16, 2018




Bodi ya Ligi ya TFF imefanyia mabadiliko ya mchezo wa ligi kuu bara kati ya Lipuli FC dhidi ya Simba SC uliopangwa kupigwa Ijumaa ya Aprili 20 2018.

Mchezo huo umebadilishiwa tarehe na sasa utachezwa Jumamosi ya Aprili 21 2018 katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Sababu za kusogezwa mbele mchezo huo ni wamiliki wa kuutumia Uwanja wa Samora kwa shughuli nyingine za kijamii.


3 COMMENTS:

  1. SIMBA NGUVU MOJA USHINDI DAIMA.Tunawatakia safari njema ya Iringa ila hakuna timu ya kuichukilia powa wakati huu. Lipuli sio timu ya kubeza na yale masuala ya Undugu baadae kwani kama kuna kitu cha kuivuruga Yanga kisaikolojia kabisa kabisa na ndoto zake za ubingwa basi ni kuendeleza wimbi la ushindi kabla ya kukutana nae.

    ReplyDelete
  2. Simba piga Lipuli kwa mabao nyumbani kwao kuzidi kuipa yanga kihoro cha kimbunga nao wakiwaaga wachezaji nyota wao ambao kila mmoja anajianika kuelekea kwenye hela

    ReplyDelete
  3. Mnyama jitayarishe kuipa yanga kichapo na mjiweke tayari katika kinyanganyiro cha nyota wao wataotafuta pakukimbilia kwenye wasikotumika bila ya malipo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic