September 29, 2020

 


MWINYI Zahera, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC amesema kuwa Simba hawatafika mbali kwenye michuano ya kimataifa ikiwa watacheza kama walivyocheza na wao.


Zahera aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/18 na 2019/20 alipigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni timu yake kuboronga michuano ya kimataifa.


Simba, Septemba 26 ilicheza na Gwambina mchezo wa Ligi Kuu Bara na kushinda mabao 3-0 ukiwa ni mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Zahera amesema kwa namna ambavyo Simba walicheza hamsini kwa hamsini na kama watacheza hivi kwenye mashindano ya kimataifa hawatafika kokote.

"Nimeona Simba ikicheza ni inacheza vizuri na inapenda kucheza mpira wa pasi, sasa ukiangalia namna ambavyo walicheza na timu yetu ni kwamba tuliweza kwenda nao sambamba mwanzo mwisho licha ya kwamba tumepoteza.

"Wana kazi kubwa ya kufanya kimataifa hasa kwa aina ya mchezo wanaocheza, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hawatakutana na timu kama hizi za kwetu, kule kuna TP Mazembe wao wanakuja muda wote hawajui habari za pasipasi ni kucheza kwa nguvu mwanzo mwisho.

"Kama mwendo wao utakuwa ni hivi basi itakuwa ngumu kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa kule kunahitaji nguvu nyingi na spidi muda wote ili kushinda." amesema.

29 COMMENTS:

  1. Mzee acha Mpira wa mdomoni. Kubali umefungwa tuu. Piga kazi babu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zahera hajafurahishwa na kitendo cha club ya simba kumpiga chini rafiki yake kipenzi na aliekuwa bosi wake kwenye timu ya taifa ya congo Ibenge. Jitahada zilifanyika za kumuondosha Sven ili Ibenge aje kuifundhisha simba kitu ambacho zahera kingemfurahisha sana pengine kunufaika vile vile. Sio kama Ibenge sio kocha mzuri ila utamuondoshaje Sven simba wakati tangu afike simba ni ubora tu wa timu kuongezeka kila kukicha? Ibenge huyo huyo kwa kusaidiwa na fitina za zahera alikuja Dar na akapigwa na simba na kikosi cha kawaida sana cha simba na simba ikasonga mbele kwenye caf champion na Vita wakibaki watazamaji. Kwa simba hii ya akina Louisi Miqisone na bwalya,Morrison na Onyango bila ya kusahau wachezaji waandamizi kama Boko ,mkude,fraga,chama na wengine wengi basi wanasimba watarajie makubwa zaidi we acha zahera aseme atakavyosema ila simba hii ipo juu na maneno ya zahera si ya kujenga bali ni ya kuwaondolea wachezaji wa simiba uwezo wa kujiamini kitu ambacho si cha kiafya katika kuwajenga wachezaji na morali ya kupambana. Tuliona simba iliofika robo fainali ya Africa na tuliziona mbinu za mpira wa Africa kwa ngazi za vilabu unavyochezwa hasa timu inapokuwa ugenini.Mbinu amabazo kama simba wamejifunza vyema kutoka wakati ule basi mara hii timu za CAF champion league zitakazokutana na simba zijipange hasa.Kwanza mfumo wa Sven huu anaotumia sasa kwa mtu mwenye akili ya mpira anajua kabisa ni mfumo unaolenga kwenda kupambana na timu zilizo na uwezo mkubwa zaidi.Yaani mfumo wa kutumia viungo wengi zaidi wenye uwezo wa kufunga magoli ni mfumo ambao simba walikosa kuwa nao na ndio uliowaadhibu kwenye magoli matano matano ya ugenini kwani magoli yale mengi yao ya vita na Alhaly na Tp Mazembe hayakufungwa na mafowadi kutoka timu pinzani bali yalifungwa na viungo wao. Na simbq ile mara nyingi ilikuwa wakikamatwa Boko na kagere kulikuwa hakuna mpango mbadala wa kufunga magoli tena, wakati huohuo akina kagere walishindwa kurudi nyuma kusaidia ulinzi na kulifanya eneo la kati kati kutamani kusaidia mafowadi zaidi kufunga mabao,yaani kama fowdi line inashindwa kumiliki mipira mbele na hawasaidii ulinzi halafu kuanza kuwatumia viungo kufanya kazi wasioandaliwa kuifanya yaani kufanga magoli hapo ndipo timu inapopotea kati kati ya mchezo na kuiachia backline kazi ya ziada. Mfumo wa sasa wa Sven ni kufunga mlango kwanza kabla ya kumfukuza mwizi kitu ambacho nnaimani kabisa kitaisadia sana simba kimataifa.kwani viungo wa simba tayari walishaandaliwa kufunga magoli ikibidi lakini jukumu la kuudhibiti mchezo ndio kazi yao ya kwanza na Sven kazi hiyo so far anaifanya vyema sana.

      Delete
  2. Huyu vipi?maandalizi ya kucheza na Mazembe Ni tofauti na maandalizi ya ligi.

    ReplyDelete
  3. Hivi tofauti ya "Set Piece " na Dead Ball" ni nini? Samahani kwa kuwatoa nje ya mada.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kitu kimoja. Kwa sababu set piece inaweza kuwa mpira wa kona au adhabu ndogo lipigwalo katika eneo karibu na goli la mpinzani

      Delete
    2. Inamaana set piece lazima iwe karibu na goli siyo. Asante kwa ufafanuzi Ndg Waziri.

      Delete
    3. Ndio. Faulo za golini kwako kuelekea goli la mpinzani haiitwi set piece, inakuwa free kick

      Delete
  4. Huyu nae akili yake imedumaa. Muda wote anaiwazia simba, shughulika na timu yako, na usisahau kuwashauri wajomba zako yanga. Kila silu mazembe, mazembe, vita, vita. Nini mazembe bwana mpira unachezwa na timu nyingi tuu. Peleka huko congo upuuzi wako

    ReplyDelete
  5. Atafika yeye na Gwambina take kama alivoifikisha Yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa wale wazee mliowasajili kimataifa subirini mle tano tano zenu

      Delete
  6. Huyo kocha Ni kiazi, kila siku anabeza team za bongo lkn yeye mbona slishindwa kuwabadili utopolo wawe nampira Kama anaowaza yeye wa mazembe na vital. Aache mdomo Kama muimba taarabu mpira hauchezwi mdomoni mpira uwanjani ndo huchezwa. Alitaka tumtungue 10 au? huwezi kutumia nguvu nyingi kwa mtoto ukajiumiza bure wakati tunamashindano makubwa zaidi mbele. Aache mdomo la sivyo akawashauri utopolo wenzake hko wanaombwelambwela mpaka leo.

    ReplyDelete
  7. Kwa akili za zahera nina hakika siku gwambina akikutana na yanga, atafanya kila juhudi gwambina wafungwe magoli kumi ili kumkomoa simba. Mtakumbuka maneno yangu. Huyu ana visasi na simba bila sababu ya maana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. True! kwa akili zake ataifanya gwambina kuwa utopolo "b"

      Delete
    2. Mnajiokotea akina biashara subirini akina TP mazembe wawaoe

      Delete
  8. Kweli mikia fc bwana mkikutana na TO MAZEMBE basi ni 10-0. Maana mnaaminisha mashabiki kuwa timu ipo levels za Al Ahly kumbe nyie wa matopeni tu, kiufupi kama ihefu mnaifunga kwa taabu sana , mnadroo na mtibwa mtaponea wapi kwa WYDADICASABLANCA?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahly, zamalek, ismailia, arab contractors, al harach, enyimba, asec mimosa, na wangine wengi tu washapigwa taifa na mnyama, na huko kwao hawajawahi kutufunga kumi ila nyie mshachezea sita barabara. Kama huna kumbukumbu bora unyamaze kwani wa utopolo

      Delete
    2. Mbona As vita club huitaji umesahau mlipokula mkono mkono?

      Delete
  9. Kama hujui mpira si lazima uchangie kwenye huu ukurasa tunachojua sisi washabiki wa Yanga wana hasira sana na simba, rejea vurugu wanazo zifanya dhidi ya washabiki wa simba, sasa mtu anakwambia simba wanaifunga IHEFU kwa tabu, mara sijui simba kadroo na mtibwa mi nakumbuka SIMBA ilifungwa na mashujaa lakini ikaingia robo fainali ya CAF, roho zinawauma kweli washabiki wa Yanga wana hasira kweli tunawakeraaaaaaaaaaaaaaa!!!!

    ReplyDelete
  10. Wewe nani? Mpumbavu huna lolote shukuru hako ka timu kamekuokota huko kongo ungekufa kwa njaa unaanza kutowa maneno peleka ujinga wako huko kwenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtu alikuwa anajitapa anaishi paris kibarua kimeota nyasi bado anazunguka Tz oh nataka kufungua akademi ya mpira alifikiri Simba wangemchukua

      Delete
    2. Ukweli unauma ila zahera kasema kweli tano tano zipo palepale

      Delete
  11. Kwani Simba Dini wapendwa isikosolewe?

    ReplyDelete
  12. Wewe mwandika INSHA ungetusaidia kwenye mambo ya kuendeleza mpira na siyo majungu utadhani ulizaliwa Bar,Hiyo makala ungemsaidia Ceo wenu asiende Misri kujua mpira, maana wewe unajua mengi hata ya hisia kAma siyo siri za watu

    ReplyDelete
  13. Tutawaona, kama na mtibwa tu jasho liliwatoka, na IHEFU wakabebwa,huko mbele safari hii sio hamsa tena itakuwa temsa.

    ReplyDelete
  14. Mikia kwa uchezaji wao wa show game kimataifa hawatoboi, ndio maana msimu iliyopita wali ishia mechi ya kwanza.
    Kama wasipo badilika wataishia walipo ishia mwaka jana kimataifa.

    ReplyDelete
  15. Zahera yupo sahihi kabisa hao mikia hawafiki mbali hata mwaka Jana tulishuhudia tano tano

    ReplyDelete
  16. Hao Simba kucheza na majukwaa tu subirini muone anavyopigwa tano tano kimataifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic