UONGOZI wa Simba leo umetoa tamko rasmi kuhusu suala la mchezaji wa Yanga, Ramadhan Kabwili, kudai kwamba aliahidiwa kupewa gari aina ya Toyota IST ili asicheze kwenye mchezo wa watani wa jadi msimu uliopita 2018/19.
Kabwili, aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio ambapo alidai kuwa alifuatwa na Simba ili afanye makusudi kupata kadi ya njano kwenye mechi yake dhidi ya JKT Tanzania ili asicheze mbele ya Simba.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Simba kupitia ukurasa wa Istagram imeeleza kuwa wanasikitishwa na kauli ya mchezaji huyo wa Yanga, Ramadhani Kabwili kwa kuishushia hadhi klabu ya Simba ambayo inazidi kujijenga kwa sasa kwenye ushindani wa soka.
"Tumepokea taarifa ya Ramadhan Kabwili wa Yanga aliyoitoa kupitia kipindi cha Radio cha East Afrika, kwa masikitiko Januari 27, ni za kusikitisha kuhusu upangwaji wa matokeo, kauli ambayo inapingwa na klabu ya Simba na kukemewa vikali.
"Tunashukuru kwa hatua iliyochukuliwa na TFF kwa kuchukua hatua na inaamini kwamba ipo kwenye yombo husika na vitachukua hatua stahiki.
"Kwa sasa klabu inawekeza nguvu nyingi kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, ligi kuu pamoja na mashindano mengine," ilieleza taarifa hiyo.
Simba kesho itashuka kesho Uwanja wa Taifa kumenyana na Namungo mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kabwili, aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio ambapo alidai kuwa alifuatwa na Simba ili afanye makusudi kupata kadi ya njano kwenye mechi yake dhidi ya JKT Tanzania ili asicheze mbele ya Simba.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Simba kupitia ukurasa wa Istagram imeeleza kuwa wanasikitishwa na kauli ya mchezaji huyo wa Yanga, Ramadhani Kabwili kwa kuishushia hadhi klabu ya Simba ambayo inazidi kujijenga kwa sasa kwenye ushindani wa soka.
"Tumepokea taarifa ya Ramadhan Kabwili wa Yanga aliyoitoa kupitia kipindi cha Radio cha East Afrika, kwa masikitiko Januari 27, ni za kusikitisha kuhusu upangwaji wa matokeo, kauli ambayo inapingwa na klabu ya Simba na kukemewa vikali.
"Tunashukuru kwa hatua iliyochukuliwa na TFF kwa kuchukua hatua na inaamini kwamba ipo kwenye yombo husika na vitachukua hatua stahiki.
"Kwa sasa klabu inawekeza nguvu nyingi kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, ligi kuu pamoja na mashindano mengine," ilieleza taarifa hiyo.
Simba kesho itashuka kesho Uwanja wa Taifa kumenyana na Namungo mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Timing ama muda wa tuhuma hizi za kabwili kwa Simba ni kitu cha kutafakakari sana. Simba imekuwa ni klabu ya mafanikio Tanzania hakuna ubishi juu ya hilo.Ni juzi tu taarifa zimetoka kuwa Simba ni zaidi ya Glasgow Rangers ya uskotiland hivi sasa kwa upande wa wapenzi na mashabiki na hata umaarufu kwenye zama hizi za utandawazi.Na ni baada ya simba kupigana kiume Africa na kupelekea Tanzania kuingiza timu nne Africa.Na licha ya Tanzania kupata nafasi ya kuingiza timu nne Africa msimu uliopita lakini kutolewa kwa Simba mapema katika mashindano ya Afica kumeirejesha Tanzania tena katika unyonge wa mpira katika ngazi za vilabu kwa kurudi tena kunako kuwakiliswha na timu mbili badala ya nne.Na ni juzi tu tumemshuhudia samata akiwa mchezaji wa kwanza wa kitanzania kucheza primier league. Unapomzungumzia samata hata kama hupendi kwakuwa kwao ni Tanzania basi lazima Simba itahusika na kitu kizuri zaidi hata yeye mwenyewe samata anathamini mchango wa Simba kufika alipo sasa. Yanga wana hasira,wana chuki ya dhahiri juu ya Simba kutokana na mambo mengi kama kukosa ubingwa wa ligi kuu kwa muda sasa,kuchukuliwa kwa wachezaji na Simba ambao walishawaekea malengo,na mambo mengine kadhaa wa kadhaa. Ila hasira za Yanga au wanayanga ukiziangalia zinapindukia na kuwa husda,uadui zidi ya Simba. Habari zozote mbaya za Simba basi kwa wanayanga ni sherehe kubwa watacheza na kujimwaya hata kama habari hizo ni madhara zaidi kwao wenyewe Yanga kuliko Simba.Mfano kutolewa kwa Simba mapema kwenye CAF championship,Yanga waliruka kwa furaha ila wanashindwa kufahamu yakwamba kuna uwezekano mkubwa kwa timu yao ikawa mtizamaji wa mashindano hayo kwa miaka kadhaa labda itokezee nafasi ya Tanzania kuingiza timu nne Africa. YANGA wana wivu na maendeleo ya Simba lakini inaonekana badala ya Yanga kutafakari nini cha kufanya ili na wao wapate maendeleo lakini inaonekana Yanga wamejikita zaidi kutaka kuibomoa simba kifitina nakadhalika. Hata habari za kabwili kamwe haiwezi kuipaka mavi Simba peke yake ni kuipaka kinyesi Tanzania kwenye medani ya soka. Kuekeza kwenye vita ya Majungu na husda kamwe hakuwezi kusaidia upande wowote ule kwa mpira wa Tanzania .
ReplyDeleteumeandika kwa hisia na uchungu tungojee haki itendeke ili mpira wetu uweze kuendelea bila ya fitina na majungu
DeleteYaani katika watu wanaotumia makamasi kufikiri mmoja ndio wewe
DeleteHata Kama haki ikitendeka Yanga hamtokuja kufika robo fainali ama nusu ya caf endeleana na kupambana na Simba tutakuja kuona mtakacho faidi
DeleteInasemekanaaa hata yule refa aliyetoa penati tata alikula mulungula... so inabidi wakanushaji waoneshe kweli hawahusiki na mbinu chafu nje ya uwanja...
ReplyDeleteKama nyie mlivyo fungwa mwaka Jana Basi Simba alihonga,lile gori la pili mlilofungwa kwa kumsukumiza shabalala mlihonga kwa refa siyo
DeletePovu rukhsaa!!!
ReplyDeleteHata Yanga alipofungwa tatu mtungi 3-0 na Kagera sugars kipa alihongwa.
ReplyDeleteSijui nikipi team ya yanga wanawaza na menejiment kazi kwao Kama kila mechi ambazo Simba anafungwa anahonga hakuna na kila mechi anayofungwa yanga Simba anahonga tff walioni mpira wa Tanzania unachafuliwa
DeleteHata Singida ya Mwigulu mchemba ilijelegeza mbele ya Yanga ili ifungwe na yanga.
ReplyDeleteTuseme hivo ,mpira hauko hivo,kumfunga as Vita ya congo licha ya kocha wao wa wakati huo mwinyi zahela kusema Simba wanatumia sumu kushinda yanga hawakusema chochote wakati wanajua ligi ya tz ndo inayochafuliwa
DeleteImenikumbusha mechi ya Simba na Mbao uwanja wa CCM Kirumba takribani misimu mitatu iliyopita wakati kiongozi mmoja wa Simba alipolazimisha kuingia chumba cha kubadilishia nguo cha timu ya Mbao wakati wa mapumziko akapambana na viongozi wa Mbao
ReplyDeleteHahahaha povu kudadeki karatasi nzima
ReplyDeleteBaada ya kukosa ubingwa miaka kadhaa wakaona njia pekee ni kununua mechi. Wanaua mpira wa Tz hawa. Tuwakemee kwa nguvu zote.
ReplyDeleteEnter your comment...ahahhaaa Sasa ist na ynga kuna uhusiano?,et Yanga inaona wivu,kmbe wivu wa ist ahahhaaa ni bora kupeleka teamu moja kihalali nuktaaaaaaaa
ReplyDeleteUnajua kwa nini Dogo amekuja kusema haya mambo kipindi hiki? Ameumia kuona dhuluma inaendelea!!! Anafungiwa yeye kucheza na kamati na wengine waliofanya makosa ya dhahiri wanaachwa!
ReplyDeleteTuache ushabiki jamani.Mpira wanaocheza simba si wa kuonga mechi. Kila mpenda mpira anafurahia.Mpaka Yanga waliona ilo mapema wakaamua kubadili kikosi mapema. Na ukiangalia kwa haraka unaona Yanga ya ushindani inaanza kuonekana. Simba na Yanga wakiwa kwenye ushindani tarajiwa unafurahia mpira.
ReplyDeleteTukubali mpira unaonekana.Ila Yanga walichelewa kidogo.
Acheni kukoloma ukweli anaujua kabwili sio nyie mikia ambao hamjui mule nini na mlale wapi kama watu wameamua kufuatlia jambo nyie majungu ya nn? Ninani ambeye hajui kuwa simba inanunua mechi au kwa sababu tff ni yakwenu!!!! Pumbavu zenu
ReplyDeleteDah sijui Malinzi atarudi lini TFF maana Vyura wanatesekaaaaaaa na badoo mtaendelea kuteseka na hata mnapofungwa na Kagera ni Simba imesaidia kuhonga.Viongozi wa Simba mnafeli wapi kuwashughulikia hawa jamaa wanaichafua brandy ya Simba?Walianza kuwa Simba inapulizia sawa kwenye vyumba na Viongozi hakumchukua hiatua za kuwashitaki walioneza hizo shutuma.Issues hizi za kusema/kuropoka kuwa Simba inahonga marefarii...kwa nini wasikamatwe na kutoa ushuhuda?Inatuumiza sana sisi wanachama/wapenzi wa Simba maana uongo huu haukemewi na hatimaye inajiaminisha ni ukweli.Shime Viongozi wa Simba chukueni hiatua ya kuwafungulia mashitaka.
ReplyDeleteHakuna Simba kuhonga wala nini Yanga tu wamechangamyikwa labda tuwanyeshe supu ya popo bawa wanaweza kukaa sawa. Alikuja Alhaly ya Misri kapigwa pale kwa makapa na Simba wenyewe wakakiri kuwa Simba sio wa kubeza hata kidogo.Alikuja sevilla ya Spain.Nasema tena Sevilla ya Spain timu inayotememesha ulaya kakini papatu na Simba kaponea chupu kwa Simba.Yanga kitu gani zaidi ya uchawi wa maneno na vitendo kwa Simba.
ReplyDeletehuyu alikataa hongo ila walipoteza mchezo na yeye akiwa golini safi sana
ReplyDeletePointi ambazo yanga wameachwa na Simba na Azam zina watesa sana.
ReplyDeletePoleni wana yanga utakuja mwaka wenu mtakuwa kileleni
Zahera kamruka Kabwili .Kabwili alidai alimweleza kocha wake.Zahera kasema akihojiwa kwamba hayawahi kusikia lolote kuhusu madai ya Kabwili.
ReplyDeleteTuache vyombo vya Sheria vifanye kazi yake, lkn mpira wa kuhonga hauna tija kataifa, hata tukitete kwa ushabiki wa kitoto.
ReplyDeleteNdio maana team zinashinda bongo lkn zinatolewa round ya kwanza mechi za kimataifa.