June 24, 2019

27 COMMENTS:

  1. Mechi za mwanzo zimetupa picha halisi ya soka letu Africa Mashariki (Kenya, Tanzania, Burundi, Madagascar, Uganda & DRC)....."pumba na mchele vimejipambanua"

    ReplyDelete
  2. Nchi hii tutaendelea kufeli kimichezo kwa ngazi ya Taifa.Tutaendelea kuwa kichwa cha muenda wazimu kwa sababu watu wenye dhamana na kufanya maamuzi kwa timu zetu za taifa hawapo makini. Amunike alishaonesha zamani sana kuwa halikuwa jaribio sahihi la kumkabidhi timu yetu ya Taifa .Tanzania kufungwa na Senegali sawa kwani kufungwa ni moja kati ya matokeo ya mpira ila kiukweli Taifa stars inacheza kana kwamba haina kocha,mpira wa hovyo kabisa hauna fomesheni ya aina yeyote.Mnaoendelea kumtetea basi endeleeni kumtetea ila kwa kweli watanzania tuliowengi wapenda mpira tunaumia sana. Uteuzi peke yake wa wachezaji ni wa hovyo kama vile haitoshi hata upangaji wa wachezaji uwanjani ni wa kutia maji. Mchezo wa mpira ni kazi ya hadharani na madudu yoyote ya hovyo yatakayofanywa kimaamuzi ofisini na viongozi husika wa mpira basi matokeo yake yataonekana uwanjani.Tanzanzia hivi sasa tuna hazina kubwa ya wachezaji vijana wa kufanya makubwa na bahati hii ya mashindano haya Afcon Misri ilikuwa lazima piga ua tuwaandae vijana wetu wa walimu waliobobea kitaaluma kwa ajili ya kwenda kuonekana duniani lakini tatizo tulipokisea ni pahala pamoja tu ni "Kocha".Huwezi kumuajiri mwalimu wa darasa la saba kwenda kufundisha wanafunzi wanaokwenda kufanya mtihani wa kidatu cha sita halafu utarajie mafanikio kwa wanafunzi wako,kamwe haiwezekani. Na huwezi kuajiri mtu wa kidatu cha sita kuwa mwalimu kwa kuwa tu amefika form six. Njnavyojua mimi licha ya course ya ualimu lakini pia lazima kuwepo na sifa kede kede nyenginezo. Lakini kwa Amunike TTF ilikosea sana na ni muendelezo wa watu wetu wa utumishi wa umma kuichukulia Tanzania very simple na kutojiamini kwamba Tanzania tuna uwezo wa kufanya makubwa. Kwanini Magufuli kachukua maamuzi ya kujenga reli ya kisasa kushinda hata mataifa mengine yenye uwezo kuliko Tanzania? Jibu ni moja tu Magufuli anajiamini yakuwa Tanzania tunaweza. Lakini Siamini kabisa yakwamba viongozi wetu wa mpira wanaimani yakwamba Tanzania tunaweza. Kuamini kwa Magufuli hakuishii hivi hivi tu halafu akaa akabweteka na kuvumilia watendaji wake wasiokuwa na viwango,hapana. Magufuli siku zote amekuwa akipambana kuajiri the best people in the job. Je TTF walipambana kutafuta the best tactician for our national team? Hapana Amunike sio miongoni mwa makocha ambao watu makini wangemkamkabidhi timu yao ya Taifa kwa ajili ya timu ya Taifa kwani hata yeye mwenyewe alitushangaa. Kule Nigeria kwao Amunike hushia kufundisha Serengeti boys wa kwao. Hawezi kufikiriwa kupewa hata nafasi ya kocha msaidizi wa timu yao taifa. Sasa kwanin sisi tumuone anafaa wakati tunashiriki mashindano sawa na timu yao ya Taifa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao vijana unaowasema wako mtaa upi? tuliandaa michuano ya vijana hapa, kilichotokea ni nini? Tungekuwa na hao vijana leo hii team zetu zingekuwa zinapigana vikumbo kuwagombania akina Niyonzima na Okwi? Tuache kujidanganya, mpira wetu bado na kikosi tulichokutana nacho jana ni kikosi bora kabisa kutoka italy, Englang, Ufaransa na Belgium huku sisi tukiwa na mchezaji mmoja tu kutoka Belgium na waliobaki wote africa tena vilabu vya kawaida sana. Tuache utani, tunahitaji mipango thabiti na sio blabla za kwamba tuna kikosi. Kipi? cha akina mkude na ajibu ambao hata hawajitambui? au cha akina Boco ambao hata soka nje ya bongo limewashinda?

      Delete
    2. Tusubiri kutolewa no count maana hatutashinda hata mechi moja.

      Delete
  3. Tuwe wakweli jamani kwa uwelewa wangu wa mpira, wachezaji wameshachaguliwa hatuna jinsi ya kubadilisha lakini suala la viungo kama Erasto Nyoni na Frank Dumayo ni bora kuliko Fay Toto. Kocha ashauriwe kwa hilo.... Haya ni mashindano sio majaribio jamani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza Erasto nyoni ni mlinzi na sio kiungo, pili frank domayo tumuangalie akiwa Azam amefanya nini? Issue ni kuwa Tz na Senegal linapokuja suala la soka hatulingani wala hatukaribiani. Tafuta vikosi halafu ndo mtajua sio tunalaumu tu.

      Delete
    2. ukifatilia,utagundua kwamba huyo ushabiki maandazi tu wa uyanga na usimba ndo unamsumbua,hana lingine lolote

      Delete
  4. Nitaendelea kuipenda Tanzania lkn kwa kocha huyu wa Timu ya Taifa...hapana.

    ReplyDelete
  5. Hapa hakuna Kocha,kikosi hakina muunganiko katikati hakuna kitu kabisa,anachelewa kufanya mabadiliko na wakati mwingine hayawi sahihi,hajui kuusoma mchezo tofauti na ilivyokuwa kwa kocha wa kenya,Kama tutaendelea hivi tutapigwa mechi zote,wachezaji hawakuandaliwa kisaikolojia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kenya wana tofauti gani na sisi? wote wamekula mbili tena kwa kukutana na vikosi bora. Tafuta kikosi cha kenya na Algeria au Tz na Senegal, huwezi kulinganisha wala hata havikaribiani. Tuache kulaumu bila kuangalia tumejiandaaje kupambana. Huwezi tegemea wachezaji wa yanga, simba na Azam wakapambane na vikosi vya England, Ufarancsa, German na Italy.

      Delete
    2. Usimtetee Amunike hana uwezo wa kufundisha natonal team..jana timu imecheza hovyo sana tofauti na Kenya ingawa wote tumefungwa 2..tujitahidi kutafuta walau sare kwa Kenya lkn algreia watatupiga nyingi tu

      Delete
  6. Waziri hana kazi ya kufanya? Kuna mambo ya kuzungumzia cyo kutolewa kwa Fei Toto, ila kama kaongea kama mshabiki ni sawa ila kama kaongea kama serikali anashusha hadhi

    ReplyDelete
  7. Watu mnaishia kulaumu tu, kabla ya Amunike mara ngapi mmefaulu kwenda Afcon? Hivi Tanzania ina wachezaji gani wa kupambana na Senegal? kwa taarifa yenu Senegal ni miongoni mwa favorite teams na ina kikosi bora kuliko timu nyingine yoyote katika mashindano haya. Senegal wanacheza mpira halisi wa kiafrica, nguvu nyingi na speed na wana wachezaji wenye misuli ya kufanya hivyo. Hatuna cha kulaumu, cha muhimu tujifunze na tuombe mungu tuweze ku-qualify kwa michuano mingine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AFCON tungecheza tu mwaka huu hata kama Monica asingekuwapo, labda kqma no yeye alihusika kupanga kundi tulilofuzu.

      Toka dunia hii iumbwe umeahawahi kuona timu inaxheza dak 90 bila kupiga shuti hata moja golini?? Kocha gani anachagua wachezaji halafu anapiga ramli ya namba za kuwachezesha? Monica hafai kabisa kuwa kocha, ni booonge la mzigo msala.

      Delete
  8. Hapa hakuna kulaumiana tanzania na senegal sawa na mbingu na ardhi

    ReplyDelete
  9. tofautisha maoni binafsi na tamko la serikali, Makamba sio msemaji wa wizara ya utamaduni na michezo. Tamko linatolewa na msemaji wa Wizara, Msemaji wa Serikali au Mtu mwenye dhamana katika eneo husika. Mzingira na Michezo wapi na wapi au ndo furahisha genge?

    ReplyDelete
  10. Makamba kazungumza ukweli kabisa kuhusu Feisal ila sio peke yake tu hata David Mwantika wote walistahiki kadi nyekundu sema refa alikuwa muungwana na siku nyingi sana sijawahi kumuona referee wa aina ile Africa ana nikumbusha referee nguli mtaliana Collina. Unajua watu wanaochukia watanzania wanaokosoa uteuzi wa Amunike kuwa kocha wa timu ya Taifa na muendelezo wake wa kazi wa hovyo ni kama vile hawaitakii mema Tanzania. Au ni watu ambao wapo very short sight of thinking kwani watanzania kama tumechelewa hata kiakili. Kuna watu wanasema hakuna haja ya kumlaumu kocha kupigwa na Senegali kwani kiviwango vya vimpira wao wapo juu zaidi? Sasa hapo ndipo panapotia kichefuchefu na kutapisha. Kama watanzania tulijua kiwango chetu cha mpira ni kidogo kuliko wenzetu huko tuendako tulifanya nini kuhakikisha tunakwenda kumechi up na wakubwa? Kwa maana hiyo sisi watanzania tumesharijiridhisha kuwa sisi ni wa viwango duni wa kudumu na ni wa kubakia huko huko katika uduni wetu yaani watanzania kwa ujinga wetu tunataka kujifanya kana kwamba unyonge ni moja ya utamaduni wetu? Mimi sikubaliani na mawazo hayo ya kishetani hata siku moja.Sisi watanzania tukiamua tunao uwezo wa kuitetemesha Africa na Dunia. Watanzania ni miongoni mwa waafrica wachache ambao wapo very resilient yaani watu ambao tukiamua kufanya letu tunafanya no matter what. Tumeamua kiswahili kuwa Lugha ya Taifa na imekuwa hivyo, wakati nchi majirani zetu wote wameshindwa kuwa na utambisho rasmi wa lugha zao za taifa kama waafrika. Tuliamua kumuondosha Idi Amini na tuliweza,tuli sacrifice au kujitolea muhanga kuhakisha nchi kusini mwa Africa zinapata uhuru na kweli kwa kushirikiana na nchi mafariki tulifanikisha hilo ila mashujaa na ushujaa uliooneshwa Watanzania kwenye harakati za ukombozi mwa kusini mwa Africa ni za kipekee. Sasa kwanini sasa hivi tumekuwa watu wa hovyo? Hata michezo pia inatushinda au wazungu kuna vitu wamevifanya vya kikachero kuuwa morali na hali ya kujiamini kwenye jamii zetu? Hatuwezi kuidharau Burundi ila wale ndugu zetu maisha ya vita na machafuko ya kikabila kwao wao ni maisha ya kawaida sasa iweje timu yao ya taifa iwe bora kuliko sisi? Kwa mpira wa miguu uchawi mkubwa na siri ya mafanikio kwa timu kufanya vizuri zaidi inategemea ubora wa kocha au mwalimu mtakayemchagua kumpa dhamana ya kuifundisha timu. Na mifano ipo mingi na hai hata hapa nyumbani. Tumeona timu ya mbao ya mwanza ilivyokuwa ikifanya vyema chini ya mrundi. Na kocha yule alipokuja kuhamia KMC ya kinondoni msimu wake wa kwanza kuifundisha timu hiyo akaipeleka kimataifa hadi Azam kuamua kumnyakuwa kuwa kocha wao mkuu.Liverpool ilitabika sana mpaka walipomleta huyu Mjerumani na sasa ni mabingwa wa ulaya. Kabla yakuja Liverpool mjerumani yule ana record za kutisha wakati akifundisha Borusia Dotmond. Hata Manchester city kabla ya Guardiola walikuwa wapo wapo tu.Ninatoa mifano hii angalau japo kama wahusika wanafahamu lakini pia kuwakumbusha mpira ni kocha na sio sehemu ya kukurupuka hata kidogo katika suala la kuteua kocha hasa wa timu ya Taifa .Kwa bahati mbaya sana Taifa stars haijafundishwa na makocha wa viwango vya Dunia kwa kipindi kirefu.Makocha wote wanaoteuliwa kuifundisha timu hiyo ni wa viwango vya chini mno hata vilabu vya Simba na Yanga na timu nyengine ndani ya ligi yetu mara kadhaa wamekuwa wakiajiri makocha wa viwango zaidi ya Taifa stars.
    Kusema kuwa wachezaji wa Simba sio muhimu ndani ya Taifa Stars na hakuna haja hata ya kuwapanga kwa wale waliopo ndani ya stars? Ila hilo ni moja ya kosa kubwa la Amunike na benchi lake la ufundi.
    Tulizungumzia kuhusu uti wa mgongo wa timu ya Taifa ya Uganda kutegemea wachezaji wa Simba.Tukazungumzia hata Saidi Ndemla pengine angelikuwa msaada mkubwa kwa taifa stars kuliko wachezaji wengi wa nafasi yake walioitwa taifa stars. Tusi zungumzie upenzi bali Wachezaji wa Simba bado wapo katika fighting spirit kuliko wachezaji wengi walioitwa taifa stars. Kuna wakati Spain walishaita wachezaji nane wa Barcelona kwenye timu yao ya taifa ila kwa kwetu tupo kisiasa zaidi na tusipobadilika tutachelewa zaidi .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo kocha Amunike ni zero kabisa.Uswahiba wake na Wilfered Kidao unatuletea majanga.Kocha hajawahi kufundisha timu yoyote ya Taifa barani Africa zaidi ya timu ya Sudan iliyomtimua kabla hata ligi haijaisha.Ameshajengeka tabia ya hovyo ya kubagua wachezaji.Kwa maoni yangu ni bora ya kumchukua kocha HANS PLUJIM au kumrejesha kocha mdenish wa timu ya vijana ambao wameshazoea mazingara ya soka la Tanzania lakini kocha Amunike ameshafeli.Aibu unapaoangalia statics Senegal possession 82% na Tanzania 18% (Manula).Na wala tusitegemee tutaifunga Kenya kwa football pattern hii ya Tanzania wanavocheza.Ningekuwa mie Kocha Amunuke ningeshatangaza kujizuulu kabla ya mashindano hayajaisha.

      Delete
  11. ha ha ha ha haaaaaaa.........hawa ndiyo Watanzania,mtu analala masikini anafikiria kuamka akiwa tajiri tena kwa lazima. nadhani mambo bado sana, ndiyo kwaaaanza tunaanza na Samatta. tusijidanganye kabisa kwa kutafuta visingizio eti angecheza fulani, nadhani mahaba kwa baadhi ya mashabiki ndiyo yanawatesa watu. sasa kila shabiki awe na kikosi chake? Nadhani soka letu bado lipo chini ndiyo tunaanza kuinukia, mpira unachezwa hadharani kila mtu anaona hapakuwa na muujiza pale wametuzidi vitu vingi sana, tukumbuke Algeria anatusubiri kwa hamu kubwa

    ReplyDelete
  12. Mambo mengine yanashangaza sana. embu tujipe mfano 1- kama kulinganisha kiwango cha Tanzania na Senegal kuwa sawa na mbingu na ardhi, huu ni unyonge uliokithiri. km mawazo yetu yatakuwa ni hayo basi niwashauri wenye mtizamo huo ama wanaotetea maamuzi ya coach basi kama hawakuona Burundi walivyocheza watazame upya marudio ya mechi ya Burundi dhidi ya Nigeria nadhani kuna kitu wataelewa na ni ni somo tosha kwa mwenye wazo kama hili. kusema kuwa Tz na Senegal viwango ni sasa na mbingu na ardhi basi vivyo hivyo kwa Burundi na Nigeria. Lakini tifautisha wenzetu Warundi walivyitoa ushindani dhidi ya Taifa kubwa kisoka. Tena nchi ndogo inayokabiliwa na changamoto nyingi.

    ReplyDelete
  13. Ukweli ni kuwa mechi ile tumshukuru refa, ingelikuwa marefa wenye msimamo wa kutoa kadi kwa makosa basi ilikuwa tupate red card at least 1. Aidha kw a mpira ule ulivyokuwa jamaa km wangelitulia ktk umaliziaji basi ilikuwa tule goli 4 au 5. jamaa wanatuzidi sawa ni sahihi kabisa ila si kucheza kihivyo. uteuzi wa coach ktk kikosi na timu kwa ujumla umetugharimu, na utaendelea kutugharimu huo ndiyo ukweli.

    ReplyDelete
  14. Ukweli ni kuwa mechi ile tumshukuru refa, ingelikuwa marefa wenye msimamo wa kutoa kadi kwa makosa basi ilikuwa tupate red card at least 1. Aidha kw a mpira ule ulivyokuwa jamaa km wangelitulia ktk umaliziaji basi ilikuwa tule goli 4 au 5. jamaa wanatuzidi sawa ni sahihi kabisa ila si kucheza kihivyo. uteuzi wa coach ktk kikosi na timu kwa ujumla umetugharimu, na utaendelea kutugharimu huo ndiyo ukweli.

    ReplyDelete
  15. Tumewatupa wazee wetu kwenye nyumba za matope, serekali haiwalipi mafaao Yao kwa wakati halafu mnapeleka hela na viwanja kwa kuwatajirisha wengine?sahauni mafanikio nchi hii

    ReplyDelete
  16. Mkulima na mfanyakazi wanafaidika kwa lipi? tumekosa radhi za wazazi wetu

    ReplyDelete
  17. Mimi nilikuwa nacheka sana nilipokuwa nikiwaona baadhi ya watu wakijipa matumaini dhidi ya Taifa stars. Kwa kutokuwa na mikakati madhubuti kwa Taifa stars hasa katika eneo la benchi la Ufundi basi ni kama tumekwenda kuwashusha thamani vijana wetu kule Misri. Na inawezekana kabisa baada ya mashindano haya Afcon Tanzania ikaporomoka zaidi katika viwango vya soka duniani na Africa. Ninaamini hata Cape Verde au lethoso wangeipata hii nafasi kushiriki AFCON wangekuwa na ushiriki wa heshima kuliko sisi Tanzania. Tumevurunda kwenye mashindano ya Africa ya Under 17 yaliyofanyika kwenye Ardhi yetu halafu tukachukulia kama vitu vya kawaida hata baadhi ya viongozi wakuu wa mambo ya michezo walionekana kutojali au kushtushwa na matokeo yale mabovu ya serengeti boys.Na sasa kule Misri kuna dalili zote yakwamba Taifa stars itayaaga mashindano yale kwa aibu lakini pia bado kuna watu wanaona kuvunda kwa Taiifa stars ni sawa tu kwa sababu sisi ni dhaifu au ni timu nyonge? Udhaifu na unyonge kwa taifa stars tumeutengeneza sisi wenyewe. Watanzania tatizo letu ni unyonge wa akili na tutaendelea kuteseka si kwenye michezo tu bali hata kwenye maisha ya kawaida .Tunahitaji mjadala mpana katika hili la Taifa stars na sio kuleta siasa.Na lazima watanzania tujenge utamaduni wa uwajibikaji kwa wahusika waliopewa dhamana na umma halafu wakalitia Taifa hasara na aibu. Tuwache ujinga wa kuchekeana panapotokea maharibiko kwa mambo ya msingi na lazima tuweke mikakati ya kujiwakilisha vyema kimataifa kwani bado kabisa Tanzania tunaonekana ni wa masihara mno katika michezo hasa kwa ngazi ya Taifa.

    ReplyDelete
  18. mafanikio ya leo ayaji hivi bila ya jana. tatizo siasa zimezidi hadi kwenye mamvo ya ufundi.
    unaposema tz tuko nyuma kimichezo basi tuseme tuko mbele kwenye nini, na tusijilinganishe na uganda na kenya,
    nafikiri tukipata watu makini katika kila nyanja wabobezi wa masuala hayo basi tutafika mbali kwenye kila jambo. muweke waziri wa habari mwenye ubobez wa mambo ya habari na michezo, muweze rais TFF mwenye kujua mpira. kila idara ikiwa na mwenye taaluma kuhusu idara hiyo bila shaka tutapiga hatua. sasa unaniweka mm niwe waziri wa sheria wakati nina PhD ya Uchumi.
    Ahsante

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic