April 5, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limejichanganya kumzuia beki wao Kelvin Yondan kwa madai ya kuwa ana kadi mbili za njano.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kwa mujibu wa rekodi zao zinaonesha kuwa Yondani hana kadi mbili na badala yake Pato Ngonyani ndiyo alipata hizo kadi.

Ten ameeleza kuwa CAF wamekosea kufanya maamuzi hayo huku akidai Yondani ana kadi moja pekee na si mbili kama walivyosema.

CAF ilituma tarifa ya wachezaji wanne wa Yanga kuzuiwa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC ya Ethiopia ambao walipewa kadi mbili za njano kila mmoja.

Wachezaji waliotajwa na CAF ni Papy Thsishimbi, Obrey Chirwa, Said Makapu na Kelvin Yondan.

Hata hivyo uongozi wa Yanga umesema utafanya mawasiliano na uongozi wa CAF ili kuona kama wanaweza wakalifanyia mabadiliko suala hilo.


8 COMMENTS:

  1. Nini maana ya tafsiri umafia??kuna haja ya kupitia kamusi kabla hujakusudia kutafuta kichwa cha habari.its a shame

    ReplyDelete
  2. Twaha utapoteza muda wako bure. Ndio waandishi wetu hawa.

    ReplyDelete
  3. Hapana siyo waandishi wetu hao. Sijakubaliana na hiyo sentensi ila ni matakwa ya mtu, uandishi si kupotosha maana ila kukoleza ama kuleta mvuto kwa neno sahihi, UMAFIA siyo sahihi kwa habari ambayo imeandikwa

    ReplyDelete
  4. Kwa nini asingesema CAF yajichanganya juu ya kadi ya Kelvin Yondani?

    ReplyDelete
  5. siku zote waandishi wetu huandika kuchonganisha ni wachochozi

    ReplyDelete
  6. Vichwa vya habari havina uhusiano na habari zenyewe

    ReplyDelete
  7. Nafikiri kuna shida kubwa inabidi wajitathimini, endapo wanataka Jamii iendelee kupenda Media

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic