April 5, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Mtibwa Sugar kesho kitakuwa na kibarua dhidi ya Singida United dhidi ya Singida United mjini Singida katika Uwanja wa Namfua.

Kuelekea mchezo huo Msemaji wa timu, Thobias Kifaru, ametamba kuwa wamejiandaa kupeleka uchungu kwa walima alizeti hao ambao walitoka kuiondoa Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Mtibwa tayari wameshafanya mazoezi yao ya mwisho mjini humo na sasa wapo tayari kwa mchezo huo wa ligi kuu bara.

Kifaru amesema hawaifoii Singida huku akitamba kuwa anaamini pointi tatu zinatapatikana Namfua baada ya dakika 90.

Mbali na mchezo huo, Kifaru pia amesema baada ya kumaliza kazi mjini Singida, kikosi hicho kitasafiri kurejea Morogoro kwa ajili ya kukipiga na Simba.

Kifaru ameeleza kuwa Simba waliifunga Njombe Mji lakini kazi watakuwa nayo pale watakapocheza dhidi ya Mtibwa Jumatatu, kwa maana wamejipanga.

SOURCE: EFM RADIO


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic