April 8, 2018



Beki wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro, amesema kuwa soka lake litabakia ndani ya Yanga kwa sababu ni nyumbani kwake.

Akizungumza mapema baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kumalizika jana dhidi ya Wolaitta Dicha SC kutoka Ethiopia, Cannavaro alieleza hayo wakati akizungumzia namna matokeo ya mchezo yalivyokuwa.

Cannavaro alisema kuwa Yanga ni nyumbani kwake na anafurahia kuendelea kuchezea hapo huku akiwataja wachezaji wengine wakongwe kama George Kavilla na Henry Joseph ambao wamedumu kwenye soka la hapa Tanzania na klabu zao kwa muda mrefu.

Yanga ilianza vema mchezo huo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiwekea matumaini mazuri ya kuelekea hatua ya makundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic