BREAKING:BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Yanga leo ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba.
Morrison mwenye mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara wakati akikipiga Yanga alikuwa kwenye mvutano mkubwa na mabosi wake kwenye suala la mkataba ambapo mchezaji alisema kuwa ana dili la miezi sita huku uongozi ukisema kuwa amesaini dili la miaka miwili.
Leo Agosti 8, Morrison amevalishwa uzi mwekundu na kuonekana akisaini dili jipya la kujiunga na Simba.
Huu unakuwa usajili wa kwanza kwa Simba kutambulishwa rasmi kwa ajili ya msimu wa 2020/21.
Thamani ya dau lake inatajwa kuwa ni zaidi ya milioni 150 ambayo amepewa ili kujiunga na klabu ya Simba huku akitajwa kupewa dili la miaka miwili.
Time will tell, amesha choka kukaa Tz anasepa na pesa za Yanga na Simba
ReplyDeletehana hela ya Yanga huyo...hakuwa na mkataba wa miaka miwili...Niyonzima asipate miwili ije iwe Morrison
DeleteSubiri tarehe 10, mbona kelele nyingi na povu kibao?
Deletebaki humo humo ndo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia hapo atukulaumu
ReplyDeleteHivi Yanga walishamalizana na Morrison huko TFF, Polisi na FIFA?
ReplyDeleteTarehe 10 Jumatatu ndiyo majibu yanatakiwa kutolewa
DeleteJamaa inaelekea hakuwa na mkataba. Kigugumizi cha Yanga katika kusema ukweli ndio matokeo yake.
ReplyDeletePicha ya Miraji Athumani pole mhariri uchungu uwa unauma bila drip
DeleteYanga baado wanasema wanamsubiri atakayethubutu kumsajili mchezaji wao sasa sijui hii imekaaje? TFF walisema wamewapa Polisi jukumu (ni lao) la kuchunguza kuhusu saini ambayo Morrison alisema ilighushiwa. Matokeo yalitolewa?
DeleteMovie ya Morrison inaendelea!!!!!! Sasa itachezwa vizuri zaidi kwani inawahusisha waliokuwa wanampa kiburi akiwa Yanga
ReplyDeleteNdio mpira wa bongo fitna ndio mpango mzima, ndio maana kimataifa hatutoboi
Deletewaache waende wajitundike kama au wakajirushe kwenye daraja
ReplyDeleteKwa hivo ni wazi jamaa walighushi saini yake na ghushi ni kosa la jinai kwahivo tunangojea matokeo yake kwa yule aliyeghushi ni crime kubwa. Aibu aibu aibu
ReplyDeleteInauma bana.Hao simba watatunyanyasa mpaka lini? Inatia hasira viongozi wetu wa yanga siwaelewi.Tutaendelea kunyanyaswa nje na ndani ya uwanja mpaka lini?
ReplyDeletetarehe 10 ambayo ndiyo siku ya hukumu bado haijafika, na wewe unawahukumu viongozi wako kutokana na kile unachokiona kwenye mitandao ya kijamii, yaani unawashinikiza viongozi wajichukulie sheria mkononi? Au wanachama wajichukulie sheria mkononi dhidi ya viongozi wao? Mi nadhani utulivu nao ni busara
DeleteKughushi saini ni wizi Mwanyeto atawwatokea nyongo. Walimtesa sana huyo kijana tazama furaha yake na huku anatia sahihi. Mungu amhukumia Molinga
ReplyDeleteMimi bado ninasubiri viongoxi wa Yanga wakiri ukweli kama Morrison hakuwa na mkataba au alikuwa nao. Mbona mara zote wamekuwa wakiwaaminisha wananchi ambao wanajinasibu ndio wenye timu yao kuwa Morrison ni mchezaji wao?
DeleteUnaamini kwamba waligushi sahihi pamoja na dole gumba?
DeleteHata huyo Mwamnyeto huenda walimtilia saini Bila ya ridhaa yake na huenda nae akakanusha kutia saini yake
ReplyDelete