August 11, 2020

 
Uongozi wa Azam FC umesikitishwa sana na tabia ya Klabu ya Yanga ambayo wamefanya leo ya kumuandikia barua mchezaji wa Klabu hiyo Salum Abubakar 'Sure boy' ya kuomba kuondoka ndani ya Klabu hiyo . 


Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC, amesema kuwa barua hiyo iliyowasilishwa leo ina makosa mengi kwani imewasilishwa na mtu wa Yanga ambaye alikuwa anapeleka barua za ofa za kumtaka Sure boy mwanzoni na imeandikwa tarehe 12/08/2020 ikiwa leo ni tarehe 11/08/2020.


Zaka amesema kuwa inaonekana Klabu ya Yanga imetengeneza barua ya Salum Abubakar na kwa kielelezo hicho inaonyesha kuwa wamefanya mazungumzo na mchezaji  ambaye ana mkataba. 

"Kitendo ambacho kinaonekana kimefanywa na Yanga kinasikitisha kwani wameandika barua ambayo imeletwa na mtu aliyekuwa akileta ofa za kumtaka mchezaji wetu hii sio sawa.

"Yanga haipaswi kuongea na mchezaji ambaye ana mkataba hivyo Yanga wamefanya makosa kwa hili Klabu ya Yanga inapaswa  itoke hadharani na kuiomba radhi Klabu ya Azam haraka iwezekanavyo kwa ilichokifanya kwani mchezaji wetu (Sure boy) ameikana barua hiyo.

22 COMMENTS:

  1. Yanga ndio zao hizo na mikataba feki na magirini kibao...dau eti milioni 20 si uenda wazimu huo

    ReplyDelete
  2. Wana njaa hao waacheni wameahindwa kuwasajili kina yondani wataweza kweli kumsajili Salum?

    ReplyDelete
  3. Yanga mbona hawajifunzi? Baadae wataanza kulialia wanaonewa, waache useahili

    ReplyDelete
  4. Hao wapelekee mbele ya sheria kama walivopelekwa wengineo kwasababu wanajuwa vizuri mchezaji Ana mkataba na hilo walilofanya ni la dharau a wala hawachagui wa kumdharau



    ReplyDelete
  5. Mtibwa nao wamekuja juu mchezaji wao Shomari Kibwana mwenye mkataba amesajiliwa kimagumashi bila kufuata utaratibu.Mwaka huu tutaona mengi.

    ReplyDelete
  6. Morisson nayeye mkia si wamemsajili ana mkataba na wao waende tff

    ReplyDelete
  7. Kweli Gongowazi ndio baba Lao na ndio mana tukashuhudia kweupe kweupe 4G Kutoka kwa Mnyama na 3G Kutoka kwa Kagera

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmeuza timu mikia nendeni mkadai hela zenu. jamaa hajalipa mpo kimya kama mazuzu jamaa anaipigia hela. Anawanunulia mechi mnaridhika. Nendeni mumdai hela zenuu ili mkanunue timu nyingine muipeleke pale msimbazi maana limebaki gofu lisije likawabomokea.

      Delete
    2. Nyani bwana kashashiba anaropoka tu eti gofu timu haina hata uwanja wa mazoezi alafu anaita jengo la Simba gofu Tumbili wanachekesha kweli

      Delete
  8. Nyani kwani huwa wana pa kulala,?Si ndio yale yale ya manyani?Hata Uwanja wa kunyooshea viungo hamna bado ngebe nyingi Luc Eymael alipaswa kupewa medali ya kusema kweli na sio kushutumiwa.

    ReplyDelete
  9. MTIBWA SUGAR WALIKUA WAPI SIKU ZOTE HIZI ? HIZI NI NJAMA ZA SIMBA ILI YANGA IONEKANE INASAJILI WACHEZAJI WALIO NA MIKATABA NA CLUB ZAO !! WANADHANI WATANZANIA HAWANA AKILI AU HAWAJUI KUZICHAMBUA NJAMA ZAO!!! AZAM WALIISIFIA YANGA KUWA WAMEFANYA UUNGWANA KUWATAARIFU KUA WANAMTAKA SURE BOY NA LEO HAO HAO AZAM WANAILAUMU YANGA !!! MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA NA MWISHO WA SIKU MBIVU NA MBICHI ZITAJULIKANA TU

    ReplyDelete
  10. sisi watanzania hua hatufikiri au vipi! unamwita mtanzania mwenzio nyani halafu unafurahi na kucheka !! sasa wanapotudharau wazungu na kutuita nyani tunakasirikia nini wakati wenyewe tumeshajidharau !! bado nashangaa sana !!

    ReplyDelete
    Replies
    1. We ushawahi kusikia mtu anaitwa mikia kweli nimeamini ile methali ya Nyani haoni kundule, mnapenda kuwauta simba mikia fc na sisi tunawaita Manyani Fc ni utani usikasirike bro kwani si ni kweli Yanga ni Manyani fc

      Delete
  11. Pelekeni fifa azam fc wafungiwe miaka 5 ili wafundishwe

    ReplyDelete
  12. Pelekeni fifa azam fc wafungiwe miaka 5 ili wafundishwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic