October 3, 2020

 


UONGOZI  wa Klabu ya Yanga leo Oktoba 3,2020 umefikia makubaliano ya kumfuta kazi kocha wao mkuu, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia aliyechukua mikoba ya Luc Eymael.

Zlatko amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara ambapo katika mechi hizo ameshinda mechi nne na kulazimisha sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.

Leo Oktoba 3 amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Coastal Union ambapo Yanga ilishinda mabao 3-0.


Taarifa rasmi iliyotolewa na Klabu ya Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya kusitisha makubaliano kwa pande zote mbili.


22 COMMENTS:

  1. Wanasema ameshindwa kuwafundisha wachezaji kupiga visigino kama Chama. Hahaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  2. Sina utaalamu ktk soka, lakini kwa hili naona taaluma ya soka inachezewa sana na Hawa ndugu zetu, hivi kosa la Mwalimu ni lipi haswa?

    ReplyDelete
  3. Waandishi wote mashabiki nao plus wachambuzi waliona kocho kashindwa fundisha timu yanga inapata matokeo kwa mpira wa ajabu

    ReplyDelete
  4. Pressure ya mchezo wa simba. Wakitaka Yanga hivi sasa kucheza kama simba wanakosea kwani simba kikosi kipo pamoja kipindi kirefu sasa. Kama simba watafungwa na Yanga basi simba itabidi ajitafakari.

    ReplyDelete
  5. Hii ajabu kabisa Jana nimeona kandambili walianza kucheza soka la kuvutia hasa kipindi cha pili,Kocha anakosa gani nyie yebo yebo?timu yenu inaonekana kuimarika siku zinavyoenda,mnaleta Kocha mpya aje Na mfumo mpya 5G itawahusu tar 18

    ReplyDelete
  6. Hii inaingia katika maajabu Saba ya Dunia

    ReplyDelete
  7. Mimi nahisi Kuna mgongano wa kimaslahi . Inawezekanaje kocha anafukuzwa baada ya kuipandieha timu kileleni mwa ligi ?

    ReplyDelete
  8. Mambo kama hayo sio mageni kwa hao jamaa. Bila ya timywa, piga, zomea, lalamika usiku na mchana na chania nguo, hiyo ndio misingi

    ReplyDelete
  9. Kocha hana kosa kimsingi focus yake kubwa ilikuwa kuhakikisha timu haifungwi kwanza na baadaye ulikuwa unaona anafanya mabadiliko ya kutafuta ushindi kwa namna yoyote.Hivyo ndivyo kocha yyte huanza kwenye timu

    ReplyDelete
  10. Utopolo mnasikitisha, kocha mechi tano za ligi hajafungwa hata moja zaidi ya sare moja kocha out? Hakika utopolo nao Kama team out kwenye kusaka ubingwa.

    ReplyDelete
  11. Hawa jamaa wanambinu zakizamani wanataka tuwapige tarehe 18 wasingizie tunakocha mpya au hatuna kocha. Msijifananishe na bingwa Simba sc, utopolo Ni utopolo na Simba Ni Simba tu wakitaifa na kimataifa. "Mtafukuzana sana tu na bdo" Bado zamu ya GSM kutimuliwa.

    ReplyDelete
  12. Kuigaiga huko huenda wamekumbuka kua simba walimuondoa uchebe wakiwa wanaongoza ligi na wakawa mabingwa kwanini nao wasijaribu

    ReplyDelete
  13. Nyie wamama kwan kuharibikiwa kwetu si ndo furaha kwenu Sasa mnatuhurumia wa nini,kukosea kwetu si ndo furaha yenu hebu furahini sasa.mishono ifungen

    ReplyDelete
  14. Wanasimba hatufurahii zaidi tanawaonea huruma, kila siku mnasajili

    ReplyDelete
  15. Hapa kweli naamini ninacho amini wagawe uwatawale .Mkumbuke mwaka Jana mliambiwa mnashinda Magoli ya Faulo tu.Mkacheza Club bingwa mkavuka na hizo faulo ,wanaowabeza wao mapema na UD songo ,Sasa wamewaingiza Tena Cha Kike mnawafata Mjue asilimia 90 Kama siyo 80 Watangazaji Fm Redio Simba ,Waandishi Magazeti/Blog Simba na wapo tayari kuyadanganya mjichanganye in favour of Simba Sasa tayari.Hongera Salehe Ally and Co mnayawezea Yanga

    ReplyDelete
  16. Wenzenu Wana mbinu zaidi hata za nje ya Uwanja kwani Kuna sheria ya kusema kwamba ushindi lazima Timu igonge pasi ndiyo mpira?na ninyi mnabase wapi Viongozi msio kuwa na Maadili mnadhani kila mcheZaji anaweza kumiliki mpira?
    Kwamba Kocha amfundishe Nchimbi acheze Kama Dilunga,?Nasema hivi mlaaniwe Waandishi na Mafarisayo wa Mpira wa Tanzania na unafiki u do the same in Politics and Football as well ,mko bias mnatumia vibaya vyombo vya habari na uandishi vibaya tunaona yanayoendelea kwenye siasa mnaandika mnayoyataka na interest zenu mpo tayari kupotosha ili mradi yenu yatimie halafu eti Ushindani aibuuuu

    ReplyDelete
  17. Wangesubiri kwanza tarehe 18 ndio wamfukuze vizuri watakavyo kula mkono 5 wajinga hao tutaomba mechi ipelekwe mbele ili walete kocha mpya then ndio tucheze wale kichapo kingine cha goli 5 wamfukuze huyo mungine kweli hawa ni vyura aka GONGOWAZI aka kandambili aka utoporo

    ReplyDelete
  18. Sasa kocha kakosa nini mmeshinda mechi zote ama wanashindwa zile pasi za visigino? Labda ndio kosa hilo utoporo kweli hamna akili

    ReplyDelete
  19. Waoga haooo! Morrison kawashinda hasira zenu zimemwangukia kocha, hakika utopolo mmedoda.

    ReplyDelete
  20. Mkamkope mkwasa au Zahara aje awafundishe kwa muda.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic