CHELSEA YATINGA FAINALI KOMBE LA FA, ITAKUTANA NA MANCHESTER
Chelsea imefanikiwa kuingia hatua ya fainali kwenye Kombe la FA baada ya kuifunga Southampton kwa mabao 2-0.
Mabao ya Chelsea yametiwa kimiani na Olivier Giroud pamoja na Alvaro Morata na kuiondosha moja kwa moja Southampton kwenye mashindano.
Chelsea sasa itakutana na Manchester United kwenye hatua ya fainali ya kombe hilo.
United iliitinga fainali mapema Jumamosi baada ya kuitwanga Totteham Hotspurs kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley.








0 COMMENTS:
Post a Comment