April 10, 2018



Mabingwa wa Zambia, Zesco wamemtangaza rasmi kocha George Lwandamina kuwa kocha wao mpya.

Lwandamina ambaye bado ana mkataba na Yanga, ameondoka bila ya kuaga na Yanga hawakuwa wakijua alipo.

Lakini Kocha huyo, ametangazwa leo rasmi kurejea kwa Zambia na kujiunga na klabu yake hiyo ambayo aliiacha na kujiunga na Yanga.

Mabingwa hao wa Zambia, wamesema wameishamalizana na Lwandamina na ataanza kazi mwezi ujao.

Aliyekuwa Kocha wa Zesco, Tenant Chembo aliamua kuachia ngazi na Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, Richard Mulenga anaonekana ndiye alifanya juu chini kuhakikisha Lwandamina anarejea.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo jioni, Zesco imesema imeamua kumrejesha Lwandamina kutokana na ubora na weledi wake kwa lengo la kuendelea kuijenga zaidi kwa upande wa wachezaji na kuboresha umoja kati ya uongoza, wanachama na mashabiki wao.

Wakati kocha mkuu amejiuzulu, msaidizi wake Emmanuel Siwale ndiye ataiongoza Zesco kesho dhidi ya Lusaka Dynamo.

3 COMMENTS:

  1. Mbona mtaka kutuvuruga wananchi

    ReplyDelete
  2. Hee leo tena mnamlilia Lwandamina?...mrudusheni Plujim

    ReplyDelete
  3. Yangaaaa!!!!ni sawa..muache aende kutafuta amani sehemu ingine. yanga imepoteza muelekeo na mategemeo kuona wachezaji wengi wa maana wanaondoka mwisho wa Msimu huu ila Yanga itakuwepo. Yanga ilikuwepo ndugu tangu na tangu. Kikubwa viongozi kusema ukweli na si kuwaachia mashabiki, wanachama na wapenzi kuendelea kusuguana. Hata inatakiwa kuwe na ile kitu inayoitwa transparency (uwazi). Lwandamina mkataba unaisha hivyo na kama watu walitaka kandarasi yake wangemuongezea mkataba mapema ila wameona hana tena sifa..kapoteza mvuto kwa timu....angalau pia uchumi unachangia. Mi naamini sidhani kama kuna kocha mvumilivu kama Lwandamina katika maisha ya sasa. Dismas Ten ni wakati wake wa kuwaambia umma wa wapenda soka nini kilichojili na nini kinajili...bila hivyo Yanga inakwenda kusambaratika. Tulijua lazima aondoke maana hata Zesco wenyewe hali yao katika mashindano haikuwa poa ndio maana wamemkumbuka mtu wao...basi hata nyie mwaweza kumkumbuka mtu wenu. Tuache uswahili swahili wa kuficha mambo...eti wamejitonesha mazoezini...Ha ha haaaa!!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic