Baada ya taarifa za Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amerejea kwao Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United, uongozi Yanga umekiri uwepo wa taarifa hizo.
Kupitia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, Salum Mkemi, amesema kuwa ni kweli taarifa hizo zimesambaa mitandaoni lakini hawana uhakika kama Lwandamina aeshajiunga na Zesco United.
Lakini ukweli kwa asilimia mia, Lwandamina ameachana na Yanga rasmi na kujiunga na Zesco.
Usiku huu, uongozi wa Yanga umekutana kulijadili suala hilo na inaonekana hakuwa akielewana na baadhi ya viongozi.
Taarifa zilitoka hivi punde kutoka Zesco United, zimethibitisha kuwa Lwandamina ameshajiunga tayari na miamba hao wa Zambia.
Lwandamina ameondoka Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwakweli yanga inatiya huruma sana imekuwa ikiandamwa kwa mkosi baada ya mkosi na huku ikiwa wachezaji wakipoteza morali
ReplyDeleteHuyo Ajibu Simba walimzuwia na kutaka kumpa milioni sabini, lakini alikataa na akaikubalia Yanga kwa milioni hamsini
ReplyDeleteFundisho kwa club zetu hizi kupenda pesa za matajiri bila ya kuangalia mustakabali wa club kwa maisha ya baadaye Young Africans walikuwa na kipindi kizuri sana cha kujipanga na kutokuwa tegemezi wa Manji alipo kuwa anajitolea tu lkn tukajisahau na kuona kama Manji ndio mwenye club yake na haitokuja kutokea akaicha yanga ktk hali hii ya sasa. Lwandamina anaondoka Young sababu ya ukata uliyo ikumbuka club. Vilabu vyetu vimekosa strategic plan za maendeleo.
ReplyDelete