Na George Mganga
Manara ambaye ni shabiki wa kutupwa wa msanii huyo, amemtaka Platnumz kufanya naye mazungumzo kesho kuhusiana na collabo hiyo aliyopanga kufanya naye.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Platnumz aliweka komenti katika moja ya posti za Manara leo akijinasibu kwa kuandika 'This is Simbaaa" yaani Hii ndiyo Simbaa'.
Manara naye alikuja kumjibu Platnumz kuwa ameshaandaa dude 'Wimbo' hivyo anaomba kuzungumza naye kwa kesho ili waweze kuandaa huo wimbo pamoja.
"Diamond Platnumz Babu kesho nitakutafuta, nina dude nimelitengeneza nataka tufanye collabo" aliandika Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment