Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, amesema matokeo ya mechi yao dhidi ya Tanzania Prisons leo Jumatatu, ndiyo yataamua ubingwa wao Bara huku wakimaliza kazi dhidi ya watani wao Yanga.
Simba inatarajia kukutana na Prisons leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Simba ambayo inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 55, kama ikishinda leo itakuwa imeiacha Yanga kwa tofauti ya pointi 11 lakini Yanga ikiwa na michezo miwili mkononi.
Kichuya amesema kuwa mechi yao na Prisons ndiyo itakayoamua ubingwa wa Simba kwa kuhakikisha wanashinda mchezo huo kwa hali na mali.
“Mechi yetu na Prisons ndiyo itakayoamua ubingwa wetu msimu huu tukifanikiwa kuwaumiza wao tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa.
“Tukimaliza mechi hiyo tunaangalia mechi ya wale wenzetu wa upande wa pili, tunahakikisha tunawafunga ili tunyakue ubingwa rasmi,” alisema Kichuya.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment