August 8, 2019


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hakuna tatizo kati ya Yanga na beki kisiki Kelvin Yondani kwani ameomba ruhusa kutokana na matatizo ya kifamilia aliyonayo.

Yondani mpaka sasa hajajiunga na wachezaji wenzake kambini, visiwani Zanzibar licha ya kukamilisha majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' huku taarifa zikidai kwamba ana mgomo wa wazi.

Zahera amesema kuwa:"Yondani najua kwamba ni mchezaji muhimu ila kwa sasa yeye yupo likizo kwani aliniomba ruhusa kuna masuala yake anashughulikia hivyo akimaliza atajiunga na timu itakaporejea.

"Nimekubaliana naye hasa ukizingatia kwamba ana mambo ya muhimu ambayo anapaswa kuyafanya akikamilisha kazi tukirudi Dar ataungana na timu hivyo kwa sasa sisi tunajiaanda naye anaendelea kumalizia matatizo yake hakuna mgomo," amesema.

12 COMMENTS:

  1. Kumbe migomo angali ikiendelea mpaka sasa. Haikuathiri kitu kwani mpaka michezo ya kujipima yote Yanga wameshinda na inaendelea kushinda Huko kisiwani tena Kwa magoli mengi sana

    ReplyDelete
  2. Yondani anaweza kufanya anachotaka Yanga na hagusiki.Mimi kama mwanayanga linanikera mwalimu anapomtafutia visingizio kila kukicha.Mbona timu ya Taifa hana matatizo ya kifamilia?Anagoma nä kola mtu anajua anagoma kwani tumemwendekeza vya kutosha.Hili lisipotatuliwa litaleta mpasuko wachezaji wengine watakapoanza kuuliza maswali.Hskuna mchezaji ambaye yupo juu ya klabu.Itakuwa kichekesho haja train na timu halafu achezeshwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha uwongo kwani Wewe na Kocha nani anajua zaidi we upo kambini,wabongo kukurupuka wa naamini hisia kuliko uhalisia!

      Guessing nyingiiiiiiii!Itakuwa upo gesti Wewe huwezi kuandika upuuzi namna na hii veve!Heeeeehaaàaheee

      Delete
    2. Acha uwongo kwani Wewe na Kocha nani anajua zaidi we upo kambini,wabongo kukurupuka wa naamini hisia kuliko uhalisia!

      Guessing nyingiiiiiiii!Itakuwa upo gesti Wewe huwezi kuandika upuuzi namna na hii veve!Heeeeehaaàaheee

      Delete
  3. Nini tafauti baina ya Kakolanya, Ajibu na Yondani na wenziwe wawili? Kakolanya alipodai tu haki yake Zahera akamtimuwa kama paka mwizi lakini Kwa Ajibu na Yondani Ni kimya. Na Pia wale wengine wawili waliogoma pamoja na Yondani mara waliajiruwa wengine badala yso. Zahera Ni Moga na ana ubaguzi mkubwa kati ya wachezaji, kumfadhili huyu na kumdharau huyu

    ReplyDelete
  4. Wacha kukurupuka.Yondani amekwenda kambini hata siku moja?Mwanayanga amesema kweli Yondani hagusiki.Ana veto poker.Anajua hagusiki.Lazima abembelezwe.

    ReplyDelete
  5. Yanga bado hakuja kutulia huo ndio ukweli.Kevin Yondani,Juma Abdul na Dante kama Yanga wangelikuwa na mipango madhubuti kutaka kufanya vuzuri hasa kimataifa basi hawa ndio wachezaji waliotakiwa kuwatunza sana.Sababu kubwa ni moja tu hawa wachezaji ndio wangeweza kuwaunganisha wachezaji wapya katika hali ya ubora zaidi. Bila ya Yondani,Ajibu,Makambo,
    Gadiel,Dante,Juma Abduli Yanga inaanza upya na inakwenda kuingia kwenye ushiriki wa aibu klabu bingwa Africa.

    ReplyDelete
  6. Uongozi utatue matatizo ya wachezaji haraka.

    ReplyDelete
  7. Yondani kwanini aje kujiunga na timu siku moja kabla ya mechi...sio kitu kizuri kwani hatujui kama hatumiwi na maadui au la? Hapa uongozi uwe makini sana Mwinyi Zahera asiwaamini sana wachezaji wa kibongo kuna network kubwa sana ya wachezaji wa ndani ambao wanaendekeza migomo kwenye mechi muhimu sasa maadui wasije kuwatumia. Mimi ningekuwa Mwinyi Zahera nawaweka pembeni wasitumike kwenye mechi

    ReplyDelete
  8. Yondani kwanini aje kujiunga na timu siku moja kabla ya mechi...sio kitu kizuri kwani hatujui kama hatumiwi na maadui au la? Hapa uongozi uwe makini sana Mwinyi Zahera asiwaamini sana wachezaji wa kibongo kuna network kubwa sana ya wachezaji wa ndani ambao wanaendekeza migomo kwenye mechi muhimu sasa maadui wasije kuwatumia. Mimi ningekuwa Mwinyi Zahera nawaweka pembeni wasitumike kwenye mechi

    ReplyDelete
  9. Niliwaambia Yondani ni untouchable.Wakurupukaji wanapinga.Atacheza akipenda na watacheza akipenda.Huu ndio ukweli.

    ReplyDelete
  10. Jamani ukweli utabaki palepale kuwa waficha taarifa tu jibu ni kwamba Yondani anadai pesa zake za usajili tena usajili wa kuongeza mkataba na ule wa awali maana alipoongeza mkataba aliambiwa hali ya timu na club kwa ujumla na yeye kwa mapenzi na mpira bas akasaini mambo yakiwa mazur watampa, cha kushangaza viongozi wakaona ni sifa kuwaleta wapya bila kuanza na wazamani ili tu mashabiki wawakubali, je ungekuwa wewe hapo ungefanyeje na hali ya club uliijua kuwa kuna pesa tena maalum kwa ajili ya usajili? hapo bado mnamlaumu Yondani badala ya kuwalaumu viongozi wanaofukia mashimo kwa takataka bila mchanga ni kwweli hilo shimo litazibika, ngoja wawaumbue na zahera nae kajiingiza kwenye propoganda za waTZ weseme ukweli buana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic