April 24, 2018



Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biblia mjini Morogoro kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Yanga.

Simba imeweka kambi sehemu hiyo tulivu kuwaweka wachezaji wake sawa kuelekea mechi itakayopigwa Jumapili ya wiki hii, Aprili 29 2018 Uwanja wa Taifa.

Taarifa zinaeleza hali ya wachezaji na morali kuelekea mechi ya watani wa jadi iko vizuri kiujumla kambini.

Wekundu hao wa Msimbazi wanajiandaa kucheza na Yanga wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kujikusanyia alama 59 dhidi ya 48 walizonazo Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic