Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera anayetarajia kuwa kocha mkuu wa Yanga, leo anatua Morogoro asubuhi hii.
Zahera anekwenda Morogoro kukiona kikosi hicho kikiwa katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba katika mechi itakayopigwa Jumapili.
Kocha huyo ambaye hadi sasa ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo, amesema bado hajasaini mkataba na Yanga.
"Bado sijasaini mkataba, nitakwenda Morogoro kuiona timu na baada ya hapo mambo mengine yatafuatia," alisema Zahera.
Kocha huyo ambaye ni mcheshi ametua nchini juzi usiku na alibaki Dar es Salaam hadi leo asubuhi alipokuwa akijiandaa kwa safari ya Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment