April 25, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi mjini Morogoro kujiandaa na mechi dhidi ya watani wao wa jadi Simba kwa ajili ya mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ya wiki hii.

Taarifa kutoka kambini zinaeleza kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi, Ibrahim Ajibu pamoja na Andrew Vincent 'Dante' wanaendelea kuimarika kufuatia kuungana na wenzao juzi Jumatatu.

Ukiachana na wawili hao, Donald Ngoma naye ameungana na kikosi cha Yanga mjini humo kujinoa kwa ajili ya mtanange huo wenye amsha-amsha kubwa katika soka la Tanzania.

Ngoma ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu, hajakuwa na msimu mzuri kutokana na kuuguza majeraha yake, kitu ambacho kimesababisha akosekane dimbani.

Aidha, Amis Tambwe naye ni mmoja wa wachezaji wanaojifua na Yanga kambini ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi ya Jumapili.

2 COMMENTS:

  1. Hivi mchezaji ambaye ana zaidi ya nusu mwaka hachezi anaweza kuwasha moto....hatakuwa na msaada wowote mechi ya jpili.

    ReplyDelete
  2. Hivi mchezaji ambaye ana zaidi ya nusu mwaka hachezi anaweza kuwasha moto....hatakuwa na msaada wowote mechi ya jpili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic