April 26, 2018




Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 194 (Azam 0 vs Njombe Mji 1). Kocha wa Azam FC, Aristica Cioba, amesimamishwa kuhudhuria mechi hadi suala lake la kumtukana Mwamuzi baada ya mechi dhidi ya Njombe Mji kumalizika litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.

Kabla ya kumtukana Mwamuzi, Kocha huyo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) kwa kupinga maamuzi kwa maneno na vitendo katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 15, 2018 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic