KOCHA PRISONS: SIMBA WALIBEBWA, PENATI HAIKUWA HALALI
Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana, Kocha wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohamed, asema penati waliyopata si halali.
Simba walipata penati mnamo dakika ya 80 kipindi cha pili baada ya mshambuliaji wao, John Bocco kudondoshwa katika eneo la hatari akiwa katikati ya mabeki wawili wa Prisons.
Mohammed ameeleza kuwa penati ile haikuwa sahihi na Simba walipendelewa tu na Mwamuzi huku akidai hawakustahili kupewa
"Kakweli maamuzi ya penati kama ile hauwezi ukatoa, haikuwa sahihi, naweza kusema walipendelewa tu maana hawakustahili kuipata" alisema.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo yaliyotiwa kimiani na John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi.
Basi Prisons futeni hilo bao ili ihasabike full time Simba 1 na Prisons 0 na point zitabaki ngapi?
ReplyDeleteSimba au Yanga zikifungwa na hizi timu utasikia refa was very fair.Tazameni marajesho ya kipyenga ktk TV Azam inayochambua maamuzi ya marefarii kama ni sa hihi au si sahihi kinachoendeshwa na Mussa Kawambwa na Othman Kazi
Ilikuwa ni penalty sababu the tackle was from behind na angemvunja mguu Bocco.
ReplyDelete