April 25, 2018


Na George Mganga

Wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga watakaokutana Jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mfahamu kwa ufupi mchezaji wa Simba, Ally Shomari anayecheza zaidi ya nafasi tano Uwanjani.

Shomari alisajiliwa na Simba kabla ya msimu mpya wa ligi (2017/18) kuanza akitokea kwa walima miwa wa Morogoro, Mtibwa Sugar FC.



Mchezaji huyo ambaye mara nyingi amekuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi kama beki namba mbili, anamudu pia kucheza nafasi zingine ikiwamo ya kiungo na ushambuliaji.

Mbali na kucheza kama beki wa kulia, Shomari ana uwezo wa kucheza nafasi za kiungo ambazo ni namba 8 na 6 ambazo hutumika kupika mipira kuwalishia washambuliaji wa mwisho.

Vilevile Shomari anauwezo wa kucheza namba 7 kama winga wa kulia ama mshambuliaji, ambapo anaweza akatumika kama mmaliziaji wa mipira ya mwisho inayotengezwa na viungo.

Ukiachana na namba mbili, mchezaji huyo anacheza pia nafasi ya ulinzi katika nafasi ya kati 'Full Back' ambayo ni namba 5 na namba 3.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic