April 25, 2018



Nyota wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Steven Gerrard, amesema kuwa anaamini kwa sasa Mshambuliaji wa timu hiyo, Mmisiri Mohamed Salah, ndiye bora katika sayari hii.

Kauli imekuja kufuatia ushindi wa jana wa jumla ya mabao 5-2 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya uliopigwa Uwanja wa Anfield.

Gerrard ameeleza kuwa Salah amekuwa na kiwango kizuri ambacho kimekuwa na faida kwa Liverpool, hivyo anamuona kuwa ni bora kwa sasa kwenye sayari hii.

Salah alifanikiwa kupachika mabao mawili dhidi ya Roma jana huku mengine mwili yakitiwa kimiani na Roberto Firmino pamoja na moja likifungwa na Sadio Mane.

Mabao hayo mawili yamemfanya Salah afikishe idadi ya mabao 43 katika msimu huu akiwa na majogoo hao wa Anfield.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic