April 3, 2018



Wakati pambano la Ligi Kuu Bara likisubiriwa jioni ya leo kati ya Njombe Mji FC dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, Kocha Msaidizi wa timu ya Njombe, Mrage Kabange, ameeleza mbinu alizoziandaa kupata matokeo.

Mrage ameeleza kuwa walilazimu kupeleka nusu kikosi mjini Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United na kubakisha kingine mjini Njombe.

Kocha huyo amesema iliwabidi wafanye hivyo ili wapate nguvu ya kupambana na Simba kwenye ligi kutokana na hali ya kikosi chao kuwa mbaya kwasababu wako kwenye mazingira ya kushuka daraja.

Taarifa zinaeleza kuwa kikosi cha Njombe kilichopelekwa Shinyanga kilikuwa na wachezaji wengi wa akiba na waliosalia Njombe walikuwa ni wale wa kikosi cha kwanza.

Uamuzi huo ulifanywa ili kuipa timu nguvu ya kupigania alama tatu muhimu dhidi ya Simba ambayo imekosa ubingwa wa ligi kwa miaka mitano sasa.

Mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Sabasaba kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni.


5 COMMENTS:

  1. hata wangebaki wote,kama uwezo hawana,watakuwa wamejinyima fulsa ya kuona miti inavyorudi nyuma tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahhahahaha,,mgonjwa anatafuta pa kufia kwa kwel

      Delete
  2. Naona kwakweli kikosi cha mnyama kiko kamili. Tunangoja kuusikia mngurumo wake

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli ni kitamu washindwe wenyewe tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic