April 23, 2018



Baada ya kushangazwa na kiwango kilichooneshwa na Simba katika mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli FC, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola, ameitaka timu hiyo kuamka zaidi.

Matola ambaye aliwahi kuwa mchezaji na Kocha Msaidizi wa Simba alishangazwa na Simba kucheza chini ya kiwango walipocheza nayo Jumamosi kwenye mchezo wa ligi.

Kocha alieleza kuwa Simba haikuwa kama ile iyocheza michezo mingine, jambo ambali lilipelekea Lipuli wakaizidi Simba katika umiliki wa mpira.

Kocha ameitaka Simba ili iweze kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga ni vema ikajipanga vizuri na kurekebisha mapungufu kadhaa ambayo yanaikabili timu haswa katika umaliziaji.

Matola aligundua mapungufu hayo walipocheza nayo, hivyo amefikia hatua ya kulishauri benchi la ufundi la Simba kuwa ni vema wakaamka mapema kabla ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi.

3 COMMENTS:

  1. Kwa hili mimi namuunga mkono Matola. Hata mimi niliona ni jambo la ajabu kiwango cha Simba katika mchezo ule na sifahamu nini kilichosababisha. Utafikiri timu kama haikujiandaa au kama vile wachezaji wapya ambao hawajafanya mazoezi kwa moja. Ni lazima ijulikane sababu na kurekebishwa mapema. Pia nashauri kuwa Salamba anafiti sana kwa timu yetu ya Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba kukosa umakini katika mchezo wa lipuli ni kutokana na pressure ya mechi ya tarehe 29 ndio maana hata okwi hakumaliza dakika 90 kwakuwa alikuwa na kadi mbili za njano yeye na manula lakini mkude hakuwepo alikuwa na kadi tatu za njano nadhani ndio sababu kubwa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic